» » Trump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini


Haki miliki ya pichaAFPImage captionTrump aikosoa China kwa kutoichukulia hatua Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump amekosoa Uchina kwa kukosa kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha kuwa Korea Kaskazini inasitisha mipango yake ya silaha za nukia.

Maoni yake yamechapishwa kwenye mtandao wa twitter siku moja baada ya Korea Kaskazini kufyatia kombora lake la pili linaloweza kusafiri kutoka bara moja hadi jingine mara ya pili chini ya muda wa mwezi mmoja.

Korea Kaskazini yajivunia jaribio la komboraKombora la Korea Kaskazini lashindwa kupaaKorea Kaskazini yarusha kombora Bahari ya JapanKorea Kaskazini yafanyia majaribio kombora jingine

Korea Kaskazini baadaye ilidai kuwa jaribio hilo linaonyesha kuwa silaha zake zinaweza kuishambulia Marekani.

Bwana Trump alisema amesikitishwa sana na Uchina na kuapa kuwa hataruhusu hali hii kuendelea.

Mnamo Jumamosi Uchina ilieleza masikitiko yake makubwa kuhusiana na kufyatuliwa kwa kombora hilo Korea Kaskazini.

Haki miliki ya pichaAFPImage captionKim Jong-un akisherehekea jaribio la kombora

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...