» » Korea Kaskazini yarusha kombora katika bahari ya Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.

Haki miliki ya pichaKOREA NEWS SERVICE
Image captionKorea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la Korea kusini.
Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan.
Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake katika meizi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.
Kombora hilo la siku ya Jumanne lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40,kulingana na Korea Kusini na Japan.
Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu lakini urefu wake umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul Stephens Evans.
Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei.
Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.
Ramani ya Korea Kaskazini na Japan
Image captionRamani ya Korea Kaskazini na Japan
Waziri anayesimamia maswala ya serikali nchini humo Yoshihide Suga aliambia maripota:Uchokozi kama huu wa Korea kaskazini hauwezi kukubalika.Tuliwasilisha malalamishi yetu na kushutumu hatua hiyo.
Rais mpya wa Korea Kusini aliyechaguliwa hivi majuzi ametaka kufanywa kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la taifa hilo.
Bwana Moon pia alikutana na rais Trump wiki iliopita, huku kiongozi huyo wa Marekani akiionya Pyongyang kwamba itapata jibu sahihi.
Kurushwa kwa kombora hilo kunajiri siku moja baada rais Donald Trump kuzungumza katika simu na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe na rais wa China Xi Jinping kuhusu Korea Kaskazini.
Viongozi hao walithibitisha jitihada zao za kuhakikisha kuwa hakuna utumizi wa nyuklia katika rais ya Korea.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...