» » Waliofariki mkasa wa moto London wafika 30


Haki miliki ya pichaPAImage captionMalkia Elizabeth ametembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.

Polisi wamethibitisha kwamba idadi ya watu waliofariki kutokana na mkasa wa moto katika jumba la Grenfell Tower magharibi mwa London imefikia 30.

Bado kuna watu wengi ambao hawajulikani walipo.

Kamanda wa polisi Stuart Cundy amesema inaaminika kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, lakini kwa sasa ni vigumu sana kubaini ni watu wangapi ambao hawajulikani walipo.

Kwa Picha: Moto wa London

Hii ni kwa sababu huenda jamaa wamepiga ripoti mara kadha, kila mmoja kivyake, kuhusu jamaa zao ambao hawajui waliko.

Amesema polisi watachunguza kubaini iwapo kulitendwa makosa ya jinai.

Malkia Elizabeth na Mwanamfalme William walitembelea kituo cha misaada ambacho kinawasaidia manusura wa mkasa huo wa moto.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Waziri Mkuu Theresa May naye amezungumza na majeruhi hospitalini, baada yake kukosolewa kwamba hakuzungumza na wakazi alipozuru eneo la mkasa Alhamisi.

Moto huo ulizuka mwendo wa saa moja usiku, usiku wa kuamkia Jumatano.

Haki miliki ya pichaEPAImage captionMaafisa wamesema hawatarajii kuwapata manusura

Mada zinazohusiana

Uingereza

Mshirikishe mwenzako 

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...