» » Urusi yadai kumuua kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdad


Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionKiongozi wa wapiganaji wa Islamic State Abu Bakr al-Baghdad akihutubia Mosul 2014

Wizara ya ulinzi ya Urusi inachunguza iwapo shambulio lake la angani nchini Syria lilimuua kiongozi wa kundi la Islamic State.

Wizara hiyo imesema kuwa shambulio hilo huenda lilimuua Abu Bakr al-Baghdad na hadi wapiganaji wengine 330 mnamo tarehe 28 mwezi Mei.

Inasema kuwa uvamizi huo ulilenga mkutano wa baraza kuu la Islamic State katika mji wa Raqqa ambao ni makao makuu ya Islamic State kaskazini mwa Syria.

Kiongozi wa IS asema hawatauachilia mji wa MosulMshauri mkuu wa kiongozi wa Taleban auawa na MarekaniMarekani:kupambana na IS ni lengo letu la kwanza

Kumekuwa na idadi kadhaa ya ripoti kuhusu kifo cha Baghdad.

Hii ni mara ya kwanza ,hatahivyo, kwamba Urusi imesema kuwa huenda ilimuua kiongozi huyo wa IS.

Vyombo vyengine vya habari vilidai kwamba kiongozi huyo aliuawa ama amejeruhiwa vibaya kutokana na mshambulio yanayoongozwa na muungano wa Marekani.

Taarifa ya wizara ya ulinzi nchini Urusi iliochapishwa na chombo cha habari kinachofadhiliwa na serikali cha Sputnik imesema kuwa makamanda 30 wa Islamic State na hadi wanajeshi 300 walikuwa katika mkutano huo wa mjini Raqqa, ilongezea.

Kanali John Dorrian ,msemaje wa muungano wa kijeshi unaongozwa na Marekani amesema kuwa Marekani haiwezi kuthibitisha iwapo Baghdad aliuawa.

Hakujakuwa na tamko lolote rasmi kutoka kwa serikali ya Syria.

Uwepo wa Baghdad haujulikani kwa muda mrefu sasa ijapokuwa aliaminika kuwa Mosul nchini Iraq kabla ya majeshi yanayoongozwa na Marekani kuanza juhudi za kuukomboa mji huo mnamo mwezi Oktoba.

Chombo cha habari cha Reuters kiliripoti kwamba anaaminika kuwa katika maficho katika jangwa badala ya kuishi mjini Mosul ama Raqqa.

Kwa mara ya mwisho Baghdad alihutubia hadharani mwaka 2014 Juni alipotangaza uongozi wa kidini mjini Mosul baada ya IS kuudhibiti mji huo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...