SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?
MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,0755683295/Watsap, instagram@mwalim_yuu, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Email@yusuphngahala@gmail.com.
SEHEMU YA 33.
Tulipoishia, Sikuamini macho yangu ninachokiona ukisikia Mbuzi kafia kwenye kibanda cha supu ndio hii. Niliinuka kwa mshangao Pale nilipomwona_________Songa nayo...........Moja kati ya watuhumiwa niliowakamata kipindi cha nyuma kidogo. Alikua ni yule nilimuhoji mpaka kumng'oa meno lakini akagoma kusema lolote, nilimng'oa mpaka kucha lakini hakusema. Yule mwanaharamu alitiroshwa baada ya mimi kupigiwa simu na kuambia kuna uvamizi sehemu. Hasira ikaniingia hata yeye aliponiona kwakua anajua muziki wangu alikua tayari kaingiwa na woga. Nilikasirika nkahisi nimemwona Zabroni na kundi lake nikamfuata nimefura huku wafungwa wengine wakiniangalia. Nikamfikia na kumtia ngumi ya uhakika chaajabu hakua tayari kupigana. Alikua mpole kuliko kawaida nilimpiga ya pili akaanguka anavuja damu. Nikamfuata pale chini na kumshindilia makonde ya halali huku nikilia.
Hakutaka hata kujibu mapigo alitulia tulii huku akisikilizia maumivu. Baada ya mda mchache askari wakaanza kunitoa niliinuka huku nina machozi na kuwaangalia wote wakasogea pembeni. Hakika nilikua kidume ndani ya jela nikaamua kumwacha na kuondoka zangu. Nilifika ninapolalaga nikalala. Mda ukasonga sana jioni ikafika sikwenda hata kuchukua chakula. Nililala mpaka siku ya pili na ndipo nikiwa pale yule mwanaharamu akawa ananfuata. Nilipomwona mishipa ya kutunza hasira ikapasuka. Sura yangu ikawa nyekundu ghafla kwasababu ya hasira. Macho yalikua afadhali hata mvuta sigara. Chaajabu ni kuwa alikuwa anakuja huku anasema samahani Yuu, nisikilize kwanza tafadhali usiniadhibu.
Nikashusha pumzi kama ishara ya kupungua kwa hasira kiasi. Kisha nikakunjua ngumi ambazo nilikua nimeziandaa kukabiliana na adui. Kisha akafika na kupiga magoti na kuanza kulia akisema Yuu nisamehe sikuwa najua nilikuwa natumikishwa mimi ndiye nilikuwa mtu wa tatu akitoka Zabroni, ni Peris na baada ya Peris ni mimi. Nilishiriki kumlawiti mwanao,nilishiriki kumuua pia na mkeo nilimbaka. Mauaji mengi mimi ndo nilikua mtekelezaji. Nakumbuka siku umenikamata umeninyanyasa na kunitesa lakini nilificha siri. Hatimaye nimegeukwa na kulipwa kifungo cha maisha jela. Nisamehee Yuu.
Aliongea kwa uchungu sana mpaka roho ya huruma ikaanza kuniingia. Nikaanza kumtuliza lakini lengo langu ilikua atulie anisimulie mambo mengi kisha nikishajua nimuue. Sikutaka kumwamini mtu tena kwani Tanzania imejaa wasaliti na wabaya. Nilimtuliza baada ya mda akaanza kunisimulia akasema. Yeye alikuwa ni mwanajeshi halali wa JWTZ, na alifukuzwa kwa Makosa ya kujaza mimba mwanafunzi. Hivyo baada ya kurudi mtaani hakua na kazi yoyote. Alijaribu kufanya kazi ndogondogo za umachinga lakini serikali ilikua ikiwafukuza kwa kisingizio eti wanasafisha jiji. Hali ile ilimfanya akose chakufanya ndipo alipoanza kuuza bangi kwa kujificha na hatimae akakutana na kundi moja la watengenezaji fedha za bandia huko jijini Mbeya.
Alifanya kazi hiyo kwa mda ndipo katika harakati za kufanya kazi hiyo akaangukia mikononi mwa Jarome Singano. Huyu ndiye mkuu wa akina Zabroni ambapo alimuapisha kwa kiapo kikali kua atatumikia kazi hiyo kwa maisha yake yote. Alikubalu kwa yote na mwisho akawa anafanya kazi na Zabroni. Pia aliongeza kuwa inaonyesha hata Jarome siyo mkuu bali kuna vigogo wa serikali wako nyuma yake kwani kuna baadhi ya wakati walikua wakikamatwa na kuachiwa kwa amri za mawaziri. Hivyo akasema huenda kuna vigogo wa serikalini wenye tamaa na mali wanawatumia majambazi hao.
Zaidi akasema hata wanasiasa wamekuwa wakiwatumia katika matukio mbalimbali ikiwemo kuvuruga mikutano ya amani kwa makusudi. Kuuwa baadhi ya wanasiasa washindani! Tanzania Tanzania wapi tunaelekea? Akaendelea kusema malipo ya kazi hii yalikuwa mazuri sana na hakupanga kuiacha mpaka kufa kwake. Kili chomfanya kuongea yale yote ni kwasababu majambazi walimgeuka. Aliongea vitu vingi sana. Akanambia kuwa hata mkuu wangu wa kituo yupo mtandaoni, polisi wa pale kituoni karibu wote. Niliumia sana kuujua ukweli na zaidi aliposema Yule mkuu aliletwa kwa makusudi kwaajili yangu lakini naye baada ya kuwakosea majambazi ndipo walipokuja kumuulia kwangu. Na muuaji alikuwa Zabroni. Nilikuwa namsikiliza kwa makini sana.
Alipomaliza akazidi kulia na kusema Yuu nifanye lolote unaloweza. Nimeshiriki kuharibu maisha yako kwa 96% Nilikuwa natumikishwa na Zabroni na vigogo hatimaye nimelipwa Jela maisha. Niliinuka na kumwambia ondoka hapa kwa ukali. Akaondoka na mimi nikaendelea kulala. Siku iliyofuata nikamtafuta nikamwambia nikitoka naenda kulipa kisasi akanichorea ramani nzuri sana. Kisha akasema Yeye pale Keko si mara ya kwanza aliwahi kuletwa mara ya kwanza akatoroka hivyo anazijua njia za kutorokea.
Akasema pia yuko tayari kunisaidia kutoka ila yeye hataki kurudi tena nje. Hivyo nikitoka yeye atarudi ndani. Nilimkubalia kisha tukapanga asubuhi ya usiku ule saa 11 alfajiri ndipo tuanze safari. Nilimshukuru sana kisha tukalala wote usiku ule. Asubuhi saa 11 tukaanza safari mdogomdogo. Ilikuwa ni chini ya Bomba la maji machafu harufu nzito sana na maji yenye kinyesi yalikua yakipita. Kila kitu kipo ndani ya akili, huk ndiko kila kitu huanzia kujua nini unataka ni hatua ya mwanzo kukipata. Hakika penye nia huwa na njia.
Sikujali mavi, wala maji machafu. Nilikuwa na lengo la kulipa kisasi kisha nirudi jela hata nifungwe maisha. Tulitembea kwa kuinama kwani tusingeweza kusimama ndani ya lile bomba. Mgongo ulikuwa unauma lakini ningefanya nini. Tulifika sehemu hivi yule Jama akasema hapa kuna mfuniko na tukitoka hapa mi narudi kwani hapa tayari tuko nje ya Jela. Ila mara nyingi huwa na walinzi hivyo kuwa makini. Nikamjibu sawa kisha nikausukuma ule mfuniko taratibu na kumwangalia yule jamaa. Woga ulikuwa umenitawala sana. Nikachomoa kichwa kidogo kisha nikachungulia nje nione kama kuna usalama mara nikasikia__________________________________________________________________________________,___________________________________________
___________________Usikose sehemu ya 34 tujue nini kilifuata. Kwa lolote nitafute kwa mawasiliano hayo ya juu. Nawapenda wote na nawakubali chao
Kumbuka Kama huna Apps ya Gsn News Download Sasa
Kesho sehem ya 34 itaendelea
Maoni ushauri tuma 0769436440
No comments:
Post a Comment