» » Serikali yatoa kibali cha kuajiri watumishi 15000 kuziba nafasi za watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki.

Waziri wa nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mh.Angela Kairuki amesema tayari serikali imeshatoa kibali cha ajira 15000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki katika zoezi lililofanyika nchi nzima la kuwabaini na muda si mrefu nafasi hizo zitajazwa.

Mh.Kairuki amesema hayo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalum Iringa mh.Rita Kabati aliyetaka kufahamu juu ya ujazwaji wa nafasi hizo ambapo amekiri upungufu huo umesababisha usumbufu mkubwa katika taasisi mbalimbali za umma hivyo kuwahakikishia wananchi  kuwa tatizo hilo litakwisha hivi karibuni.

Katika hatua nyingine akijibu swali la Mbunge wa Mtwara mjini Mh.Maftaha Abdallah Nachuma aliyetaka uboreshwaji wa bandari ya Mtwara kwa kudai kuwa imesahaulika licha ya kuwa na kina kirefu katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati,Naibu waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mh.Edwin Ngonyani amesema serikali inampango wa kuboresha na kuendeleza bandari zote nchini ikiwemo bandari ya Mtwara ili kuipunguzia mzigo bandari ya Dar es Salaam.

Mh.Ngonyani amesema kuwa tayari serikali imeshatenga fedha kwaajili ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mtwara yenye urefu wa meta 350 itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni137 inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi 21.



Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS



tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...