» » Mfanyabiashara Afikishwa Mahakamani Kwa Kukutwa na Sare 5000 za JWTZ

Mfanyabiashara  wa Kariakoo, Casto Ngogo (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa na vifaa vya serikali ambavyo ni suruali 5,000 sare za Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Ngogo ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Hamisi Saidi.

Akisoma mashitaka, Wakili Saidi alidai Juni 15, mwaka huu maeneo ya bandari kavu ya Galco iliyopo Chang’ombe wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) za thamani ya Sh milioni 59 mali ya serikali bila kuwa na kibali.

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo upande wa mashitaka ulidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba hawana pingamizi ya dhamana. 

Hakimu Nongwa alitaja masharti ya dhamana kwa mshitakiwa kuwa na fedha taslimu Sh milioni 30 au hati ya mali isiyohamishika ya thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 10 kila mmoja. 

Ngogo alitimiza masharti hayo na kuachiwa huru ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn news

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...