» » Kundi la Islamic State lasema lilihusika na shambulio London

Polisi wakisaka nyumba mashariki mwa London

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi wakisaka nyumba mashariki mwa London
Polisi nchini Uingereza wamekuwa wakifanya msako kwenye makazi manne mjini London hadi usiku wa manane kama sehemu ya uchunguzi juu ya shambulio la Jumamosi ambapo watu saba waliuawa na wengine wapatao hamsini walijeruhiwa .
Wachunguzi wanajaribu kubaini ikiwa wanaume watatu walioendesha basi lao dogo na kuwagonga wapita njia kabla ya kuwachoma visu wengine wengi walipata msaada wowote.
Watu kumi na mmoja wanashikiliwa kufuatia uvamizi wa polisi mashariki mwa London.
Image captionPolisi wa kupambana ugaidi London
Kundi la Islamic State limesema lilihusika na shambulio hilo.
Mwanamke mmoja raia wa Canada aliyeuawa katika shambulio la London ametajwa katika vyombo vya habari.
Taarifa ya familia yake imesema kuwa alikuwa akifanya kazi katika hifadhi ya wasio kuwa na makazi kabla ya kuhamia Ulaya kuishi na mchumba wake.
Watu 21 waliojeruhiwa katika shambulio hilo wako katika hali mahututi.
Image captionWatu saba waliuawa kwenye shambulizi hilo




Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles