» » Huyu ndie mmiliki wa Kampuni ya dhahabu aliye kubali kujadiliana na Tanzania kuhusu malipo

Rais Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton ikulu mjini Dar es Salaam.

Haki miliki ya pichaIKULU, TANZANIA
Image captionRais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu nchini humo.
Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili kulipa fedha ambazo Tanzania inasema imezipoteza kutokana na kampuni hiyo kuendesha shughuli zake nchini humo.
Taarifa kutoka ikulu inasema hayo ni miongoni mwa mambo ambayo yameafikiwa katika mkutano kati ya Mwenyekiti wa Barrick Gold Corporation Prof. John L. Thornton na Rais John Magufuli.
Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Serikali inakaribisha mazungumzo hayo na itaunda jopo la wataalamu watakaofanya majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation ili kufikia makubaliano ya kulipwa fedha zinazodaiwa na namna kampuni hiyo itakavyoendesha shughuli zake nchini maslahi ya pande zote mbili.
Mazungumzo kati ya wawili hao yalihudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba Prof. Palamagamba Kabudi.
Rais Magufuli amesema pamoja na kukubali kulipa fedha zinazodaiwa Prof. Thornton amekubali kushirikiana na Tanzania kujenga mtambo wa kuchenjulia dhahabu nchini humo.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


ONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...