» » Walioambukizwa Ebola DR Congo wafikia 29


Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMkurupuko mbaya zaidi wa Ebola ulitokea 2014-2015 Afrika Magharibi

Idadi ya watu ambao wamashukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepanda na kufikia 29.

Idadi hiyo imepanda kutoka 21 kwa mujibu wa msemaji wa Shirika la Afya Duniani Christian Lindmeier ambaye amenukuliwa na shirika la habari la Reuters.

Watu watatu wamefariki kutokana na ugonjwa huo kufikia sasa, na wengine 416 ambao walijumuika na waliokuwa wameambukizwa wanatafutwa kuchunguzwa iwapo wana dalili za ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola waripotiwa DR Congo

Watu walianza kuugua tarehe 22 Aptili katika mkoa wa Bas-Uele kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Eneo hilo lililoathirika linapatikana kilomita 1,300 (maili 800) kaskazini mashariki mwa Kinshasa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati, eneo lenye misitu.

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles