» » Trump: Sichunguzwi na FBI

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais Trump anasema kuwa hachunguzwi

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.

Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.

Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa ISClinton: Nalaumu FBI na wadukuzi wa UrusiMkurugenzi wa FBI apinga madai ya Trump kuhusu Obama

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump aliambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia ,huchunguzwi.

''Najua sichunguzwi'', Bwana Trump alimwamabia aliyekuwa akimhoji, akirejelea madai aliyotoa katika baraua ya Jumanne ya kumfuta kazi bwana Comey.

Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...