» » Marekani yaujaribu mfumo wa kutegua makombora



Mfumo wa kutegua makombora wa Marekani ICBM

Haki miliki ya pichaMISSILE DEFENSE AGENCY
Image captionMfumo wa kutegua makombora wa Marekani ICBM
Marekani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuufanya majaribio mfumo wake wa kudungua makombora ya masafa marefu ICBM kulingana na maafisa.
Mfumo huo wa ardhini uliwekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini California na kudungua kombora la masafa marefu kulingana na kitengo cha ulinzi wa makombora MDA.
Pentagon imesema kuwa majaribio hayo yalikuwa yamepangwa muda mrefu uliopita, lakini yanajiri huku kukiwa na wasiwasi mkubwa na Korea Kaskazini.
Majaribio hayo yamefanyika baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la tisa mwaka huu.
Mkurugenzi wa kitengo hicho cha ulinzi wa makombora Admirali Jim Syring amesema kuwa jaribio hilo ni hatua muhimu.
''Mfumo huu ni muhimu kwa ulinzi wa taifa letu na jaribio hili ni thibitisho kwamba tuna uwezo mkubwa dhidi ya tishio'', alisema siku ya Jumanne.
Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Image captionUwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Lilikuwa jaribio la kwanza dhidi ya kombora la masafa marefu kwa mfumo huo wa ardhini GMD.
Mfumo huo ulirushwa kutoka Kwajalein Atoll katika kisiwa cha Marshal juu ya anga ya Pacific, kitengo hicho kilisema katika taarifa iliotolewa.
Tangazo hilo linajiri baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la tatu katika kipindi cha wiki tatu.
Kombora hilo lilisafiri kwa urefu wa kilomita 450 kabla ya kuanguka katika maji ya Japan.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...