» » Huenda nimekuwa ''dikteta'' mzuri Museveni


Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kuwa huenda amekuwa 'dikteta' mzuri kwani wananchi wamekuwa wakimchagua kwa miongo mitatu.
Image captionRais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amesema kuwa huenda amekuwa 'dikteta' mzuri kwani wananchi wamekuwa wakimchagua kwa miongo mitatu.
Raia nchini Uganda wamekuwa wakisambaza mahojiano ya hivi karibuni ya rais Museveni na shirika la habari la Aljazeera ambapo alizungumzia maswala kadhaa.
Katika mahojiano hayo, alitetea kipindi chake cha miongo mitatau kama rais wa Uganda na kuwashutumu wale wanaomuita dikteta, akisema kuwa huenda amekuwa dikteta mzuri kwa sababu amekuwa akichaguliwa na wananchi mara tano.
Alizungumzia kufungwa kwa mwanaharakati Stella Nyanzi ambaye anazuiliwa kwa kumuita, ''makalio'' akisema kuwa hana haki ya kuwatusi wengine.
''Iwapo wewe ni mwanaharakati na unafanya makosa ,kwa sababu katika kupigania haki za binaadamu pia unafaa kuzungumzia haki za wengine, huwezi kuvunja haki za wengine na kusema kuwa ni haki yako kuwatusi watu hapana.Haki zinaenda sambamba na majukumu, iwapo unajua chochte kuhusu demokrasi. Alikataa kuingizwa katika mazungumzo ya vita vilivyokuwa katika jimbo la magharibi la Kasese,ambapo vikosi vya usalama vilikabiuliana na walinzi wa mfalme wa eneo hilo, mzozo uliowacha makumi kufariki na wengine wengi kuuawa akisema kuwa ni swala ambalo linaangaziwa mahakamani''.
''Swala hilo liko mahakamani na kulingana na mahakama, wakati kitu kinapokuwa mahakamani sifai kuzungumzia. Mahakama itatuambia iwapo watu hao walikamatwa kwa sababu fulani ama la''.


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles