» » Uturuki: Trump ampigia simu Erdogan kumpongeza


Uturuki: Trump ampigia simu Erdogan kumpongeza



Nje ya makao makuu ya chama cha AK 16 Aprilu 2017Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWafuasi wa Bw Erdogan walisherehekea matokeo mjini Istanbul

Rais wa Marekani Donald Trump amempigia simu Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na kumpongeza kufuatia ushindi wake kwenye kura ya maoni iliyoandaliwa Jumapili kumuongezea mamlaka.
Rais huyo pia alimpongeza Erdogan kwa kuunga mkono shambulio la Marekani la makombora katika uwanja wa ndege za kivita za Syria mnamo 7 Aprili.
Matokeo yaliyotangazwa baadaye Jumatatu yalionesha asilimia 51.4 ya waliopiga kura waliunga mkono marekebisho ya katiba yaliyokuwa yamependekezwa.
Bw Erdogan alipuuzilia mbali shutuma kutoka kwa waangalizi wa kimataifa kwamba alipendelewa na "kampeni ambazo ziliegemea upande mmoja".
"Mnaifahamu nafasi yenu," aliwaambia waangalizi.
Ushindi wa Bw Erdogan, kwa kura chache, uliidhinishwa na tume ya uchaguzi ya Uturuki licha ya kuwepo madai ya udanganyifu ambayo yaliibuliwa na upinzani.
Hayo yakijiri, Uturuki imeidhinisha kuongezwa kwa hali ya hatari kwa miezi mitatu.

Kura Istanbul.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWapiga kura walikuwa wanaamua 'Ndio' au 'La' kuunga mkono au kupinga marekebisho hayo

Hali ya hatari, iliyotangazwa baada ya jaribio la mapinduzi ya serikali lililofeli Julai mwaka jana, ingemalizika katika kipindi cha siku mbili zijazo.

Gani jipya ndani ya katiba mpya?

  • Rasimu inasema kuwa uchaguzi ujao wa rais na bunge utakuwa tarehe 3 Novemba 2019.
  • Rais atashikilia usukani kwa miaka mitano, na hatapitisha vipindi viwili.
  • Rais ataweza kuchagua maafisa wa juu serikalini wakiwemo mawaziri.
  • Ataweza kuwapa kazi naibu rais mmoja au marais kadhaa.
  • Nafasi ya waziri mkuu ambayo kwa sasa inashikiliwa na Binali Yildirim, itafutwa.
  • Rais atakuwa na nguvu za kuingilia kati mahakama, ambayo Bw Erdogan ameikashifu kwa kuathiriwa na Fethullah Gulen, mhubiri kutoka Pennsylvania anayemlaumu kwa mapinduzi yaliyofeli Julai.
  • Rais ataamua iwapo ataweka hali ya hatari nchini au la.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...