» » Upinzani Venezuela kuandamana tena

Upinzani Venezuela kuandamana tena


kumekua na mapambano kati ya waandamanaji na Vikosi vya kuzuia ghasiaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionkumekua na mapambano kati ya waandamanaji na Vikosi vya kuzuia ghasia
Ghasia na kufyatua risasi kulijitokeza baada ya mamia ya raia wa Venezuela walipoandamana mitaani wengine wakimuunga mkono rais Nicolas Maduro na wengine wakiipinga serikali.
Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani mjini Caracas, ambapo kijana mmoja alipigwa risasi na kupoteza maisha.
Katika Mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka vurugu.
Upinzani unataka uchaguzi mpya wa urais kutokana na kudorora kwa uchumi nchini humo.
Rais Maduro ameulaumu upinzani kwa kusababisha vurugu.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema rais Maduro anakiuka Katiba ya Venezuela
Wapinzani wa rais wa Venezuela, Nicolas Maduro wameitisha maandamano mapya siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kutokea ghasia.
Kiongozi mkuu wa upinzani Henrique Capriles amezungumza na waandishi wa habari kuwa siku ya leo watakutana raia wote wa Venezuela wakiwa na lengo la kushinikiza rais Maduro kuondoka madarakani.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles