» » Rais wa Somalia atoa msamaha kwa al-Shabab

Rais wa Somalia atoa msamaha kwa al-Shabab

Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" ametangaza vita dhidi ya kundi wa wanamgambo la al-Shabab.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" ametangaza vita dhidi ya kundi la wanamgambo la al-Shabab.

Ametoa pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.

Hi ni baada ya shambulizi la kujitoa mhanga kutokea karibu na jengo moja la serikali mjini Mogadishu ambapo watu 7 waliuawa pamoja na misururu ya kutekwa nyara kwa wafanyakazi wa kutoa misaada katika taifa hilo linalokumbwa na ukame.

Rais mpya wa Somalia Mohamed Farmajo akabidhiwa mamlakaMohamed Farmajo ashinda urais SomaliaJe, Mohamed Farmajo ni nani?

Mashambulizi yamekuwa ya mara kwa mara na vikosi vyote nchini Somalia vimekuwa katika hali ya tahadhari ili kukabiliana na tisho lolote kwa usalama.

Pia amesema kuwa amewafanyia mabadiliko maafisa wa vyeo vya juu kwenye idara ya ujasusi na polisi ili kujiandaa katika vita dhidi ya al-Shabab.

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRais ametangaza pia msamaha wa siku 60 kwa wanamgambo hao, akiwataka kujisalimisha, ili wapate mafunzo, ajira na elimu.

Mshirikishe mwenzako 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles