» » Mwizi sugu wa simu Marekani anaswa kwa kutumia Apps

Mwizi sugu wa simu Marekani anaswa kwa kutumia App

Haki miliki ya pichaINDIO POLICEImage captionSimu zaidi ya 100 zilizokuwa zimeibiwa zilipatikana

Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani.

Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My iPhone kufuatilia simu zao.

Simu hizo zilikuwa zimeibiwa katika tamasha la muziki la Coachella katika jimbo la California, polisi wamesema.

App hiyo huonesha ilipo simu ya mtu, na baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kupiga ripoti kwa polisi, maafisa walifuatilia kwa kutumia app hiyo hadi wakamnasa mshukiwa.

Walipata zaidi ya simu 100 zikiwa kwenye mfuko wa mshukiwa huyo wa wizi.

Simu mpya ya iPhone isiyotumia headphoneUdhaifu mkubwa wagunduliwa kwenye simu za iPhone

Baadhi ya simu zilirejeshewa wenyewe papo hapo.

Nyingine zimekabidhiwa kwa wasimamizi wanaokusanya mali na bidhaa zilizopotea wakati wa tamasha hilo.

Polisi walikuwa tayari wametumwa kwa wingi katika tamasha hilo baada ya visa vya wizi wa simu kuongezeka, anasema afisa wa polisi Dan Marshall, akinukuliwa na mtandao wa Gizmodo.

Lakini wenye simu ndio waliosaidia kunaswa kwa mshukiwa.

Wanaohudhuria tamasha hilo wameshauriwa:

Kutoweka vitu vyao vya thamani katika mifuko yao ya nyumaKuhakikisha vitu vyao vya thamani hawaviweki pamojaKubeba pochi bandia ili kuwahadaa wachopozi

Mada zinazohusiana

TeknolojiaMarekani

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles