» » Mapya: Jiwe kubwa lapita karibu na Dunia

Mapya: Jiwe kubwa lapita karibu na Dunia

2014 JO25Haki miliki ya pichaNASA/JPL-CALTECH/GSSR
Image captionMseto wa picha 30 za asteroidi hiyo kwa jina 2014 JO25 zilizopigwa na mtambo wa Nasa
Asteroidi kubwa ambayo inakadiriwa kuwa na ukubwa karibu sawa na wa wa Jiwe la Gibraltar imepita salama karibu an Dunia.
Asteroidi hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na kipenyo cha karibu kilomita moja, ilipita karibu na dunia umbali wa mara tano hivi umbali kati ya Dunia na Mwezi.
Jiwe hilo ambalo limepewa jina 2014 JO25, ndilo kubwa zaidi kupita karibu na dunia tangu 2004.
Wataalamu wa anga za juu walisema fursa nzuri zaidi ya kutazama asteroidi hiyo angani itatokea Jumatano usiku.
Picha za mitambo ya rada zilizopigwa kwa kutumia antena ya Shirika la Anga za Juu la Marekani (Nasa) iliyo na urefu wa 70m (230 ft) katika kituo chake California zilionesha kwamba jiwe hilo lenye umbo la njugu linazunguka mara moja kila baada ya saa tano.
Jiwe hilo lilikuwa na ukubwa sawa na wa GilbratarHaki miliki ya pichaEPA
Image captionJiwe hilo lilikuwa na ukubwa sawa na wa Gilbratar
Asteroidi hiyo iliipita Dunia katika umbali wa kilomita milioni 1.8 (maili 1.1 milioni) saa 13:24 BST mnamo Jumatano, 19 April.
Inakadiriwa kwamba jiwe jingine kupita karibu na dunia itakuwa mwaka 2027 pale asteroidi ya kipenyo cha karibu mita 800 (nusu maili) iliyopewa jina 1999 AN10 itapita karibu na dunia umbali sawa na wa mwezi kutoka kwa Dunia, takriban 380,000 km (maili 236,000 ).


Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles