» » Jeshi la Magereza Lajitosa Kujenga Viwanda Vya Sukari na Viatu

Jeshi la Magereza Lajitosa Kujenga Viwanda Vya Sukari na Viatu

Wakati Taifa likijielekeza kwenye ujenzi wa Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati, Jeshi la Magereza nchini linatarajia kujenga upya kiwanda chake cha viatu cha Karanga na kuanzisha kiwanda kipya cha sukari katika Gereza la Mbigiri mkoani hapa.
 
Awali, Kiwanda cha Karanga kilichopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro kilishindwa kuendelezwa.
 
Ili kufanikisha hilo, tayari Shule ya Sekondari ya Bwawani inayomilikiwa na jeshi hilo imeanzisha mtalaa wa masomo ya sayansi ili kuandaa vijana wa kufanya kazi viwandani. 

Kamishna wa Utawala na Fedha wa Magereza, Gaston Sanga alisema mikakati hiyo inalenga kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kutilia mkazo ukuaji wa uchumi kupitia viwanda.
 
Alisema taaluma inayotolewa shuleni hapo itakwenda sambamba na mahitaji ya wataalamu watakaotumika katika viwanda hivyo.
 
“Tumeona tuanzishe mchepuo wa masomo ya Sayansi yaani CBG (Kemia, Bailojia na Jiografia) kuanzia mwakani katika shule yetu ya Bwawani,” alisema kamishna huyo.
 
Alifafanua kuwa wameanzisha masomo hayo ili kupata wataalamu wengi watakaovisaidia viwanda vya jeshi na vingine vilivyopo nchini.
 
Kamishna Sanga alisema katika kuimarisha na kujenga upya kiwanda cha viatu na kile cha sukari, wanashirikiana na mifuko ya hifadhi za jamii ya PPF na NSSF.
 
Kuhusu Shule ya Sekondari ya Bwawani, alisema maendeleo ya kitaaluma yanategemea miundombinu ya madarasa, maabara, maktaba na ubora wa afya ya mwanafunzi.
 
Alipongeza jitihada zinazofanywa za kukamilisha kuendeleza miradi mbalimbali katika shule hiyo ili kuboresha maendeleo ya kitaaluma.
 
Pia, alisema ni vyema wazazi wawe mstari wa mbele kulipa ada kwa wakati ili kuwaruhusu wanafunzi kurudi shule mapema na walimu waweze kwenda sambamba na mitalaa iliyopo.
 
Kamishna Msaidizi wa Magereza, Emmanuel Lwinga ambaye pia ni mkuu wa sekondari ya Bwawani, alisema pamoja na jitihada za ujenzi wa nyumba mbili za walimu kwa mfumo wa kujitolea na madarasa mawili, bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa jengo la utawala na nyumba za watumishi.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...