» » Donald Trump: aadhimisha siku 100 kwa kushambulia wanahabari

Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.

Image captionRais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.
Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.
Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama 'Correspondents diner' iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo.
Hafla hiyo ni miongoni mwa hafla maarufu sana mjini Washington.
Akihutubia umati mkubwa katika jimbo la Pennsylvania, Rais Trump amelinganisha na kutofautisha, kile ametaja 'siku mia moja za wanahabari kushindwa na kazi yao', na mafanikio yake ambapo amesema amekuwa akitimiza 'ahadi zake kila siku', hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta ya makaa ya mawe.
Pennsylvania ni jimbo linalotegemea uchumi wa uchimbaji madini, na lilikuwa muhimu sana katika uchaguzi wa mwaka jana.
Awali maelfu ya watu waliandamana nchini Marekani dhidi ya utawala wa rais Trump na msimamo wake kuhusu mazingira.

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles