» » Wikileaks: CIA inatumia runinga kupeleleza

Wikileaks: CIA inatumia runinga kupeleleza


Shirika la ujausi cha CIA nchini MarekaniHaki miliki ya pichaINPHO
Image captionShirika la ujausi cha CIA nchini Marekani
Mkuu wa kamati ya intelijensia katika bunge la Marekani ametaja kuchapishwa kwa stakabadhi za siri na mtandao wa Wikileaks kuwa kosa baya sana.
Devin Nunes alisema kuwa amekasirishwa sana na uvujaji wa habari uliochapishwa na mtandao huo hiyo jana unaodai kuonyesha vifaa vinavyotumiwa kudukua mitambo ya mawasiliano inayotumiwa na CIA.
Stakabadhi hizo ambazo hazijathibitishwa na makundi huru zinatoa vifaa au programu inayoweza kuchunguza simu za rununu za kisasa, kompyuta au hata runinga.
CIA na Ikulu ya White House zimekataa kusema lolote kuhusiana na mtandao huo.
Shirika la ujausi cha CIA nchini MarekaniHaki miliki ya pichaINPHO
Image captionShirika la ujausi cha CIA nchini Marekani
Vifaa hivyo vinavyodaiwa kutumika kama silaha za mtandao vinasemekana kuwa ni pamoja na programu yenye uwezo wa kuchukua ama kuharibu taarifa kwenye kompyuta zenye programu za Windo , Android, iOS, OSX na kompyuta za Linux pamoja na mifumo ya intaneti.
Baadhi ya programu hizo zinaripotiwa kutengenezwa ndani ya nyumba , lakini shirika la Uingereza la Mi5 linasemekana kusaidia kutengeneza nyaya za upelelezi zinazoweza kushambulia televisheni za Samsung.
Msemaji wa CIA hakuweza kuthibitisha taarifa hizi.
"hatutoi kauli juu ya mambo yasiyoaminika ama taarifa za nyaraka zinazodaiwa kuwa ni za ujasusi," alisema.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza hakuweza pia kutoa kauli yake kuhusiana na taarifa hii.
Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian AssangeHaki miliki ya pichaHUW EVANS PICTURE AGENCY
Image captionMwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange
Wikileaks imesema kwamba vyanzo vyake vilishirikisha umma ili kuchochea mjadala juu ya iwapo uwezo wa udukuzi wa CIA ulipita kiwango cha wajibu na mamlaka yake.
Kulingana na mwandishi wa BBC wa maswala ya usalama Gordon Corrora, taarifa hizo za sasa zilizotolewa- zinaonekana kutoa maelzo zaidi ya matumizi ya njia za teknolojia ya kiwango cha juu .
Ni suala la aibu -kwamba shirika ambalo kazi yake ni kuiba siri za watu halijaweza kutunza siri zake lenyewe.
Cororra amesema kuwa kutakuwa na hofu ya kupoteza maeneo ya ujasusi hususan walengwa ambao wanaweza kubadilisha mienendo yao kwasababu sasa wanafahamu nini majasusi wanaweza kufanya.
Halafu kutakuwa na maswali juu ya ikiwa uwezo wa kiufundi wa CIA ulikuwa mpana sana na wa siri.
Kwa sababu nyingi kati ya nyaraka za awali zilielezea uwezo wa CIA wa kulenga vifaa vya wateja, maswali makuu yanaweza zaidi kuwa juu ya nini kinachofahamika kama tatizo la ''usawa''.
Inadaiwa kuwa wapelelezi hao wamekuwa wakishirikiana na watengenezaji wa tv za SamsungHaki miliki ya pichaSAMSUNG
Image captionInadaiwa kuwa wapelelezi hao wamekuwa wakishirikiana na watengenezaji wa tv za Samsung
Hii hutokea pale unapobaini udhaifu katika sehemu ya teknolojia unayotumia, je unawezaje kuweka uwiano juu ya faida ya umma kwa kuwafahamisha watengenezaji wafunge teknolojia yao na kuboresha usalama wa kila mtu kwa faida ya shirika la upelelezi ya kuiacha ili iweze kutumiwa kukusanya taarifa za ujasusi.
Shirika la usalama wa Taifa nchini Marekani (NSA) tayari limekwisha kabiliwa na maswali juu ya ikiwa ina uwiano huu inavyotakikana wakati nyingi kati ya siri zake zilipofichuliwa na Edward Snowden, na sasa huenda ikawa zamu ya CIA .
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en


tupe maoni yako

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...