» » Watafiti wafanya ugunduzi mwengine kuhusu mti mrefu Afrika

Watafiti wafanya ugunduzi mwengine kuhusu mti mrefu Afrika

Image captionMti mrefu zaidi barani Afrika

Siku chache baada ya wanasayansi kubaini mti mrefu zaidi barani Afrika katika Mlima wa Kilimanjaro nchini Tanzania sasa wataalam hao wamefanya ugunduzi mwengine kuhusu mti huo.

Wataalam hao kutoka chuo kikuu cha Beyreuth Ujerumani sasa wamegundua kwamba mti huo ndio ulio na miaka mingi zaidi duniani.

Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania, Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo hicho Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti huo ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.

MATANGAZO

Mti huo unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, na upo katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa).

Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.

Mti mrefu zaidi Afrika wagunduliwa TanzaniaUtamaduni wa kutoa majina Afrika: Njia tisa za kumpatia jina mtoto wako

Kulingana na gazeti hilo la mwananchi ,Amesema kwamba katika utafiti walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.

Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.

Mhifadhi Mkuu wa Kinapa, Betrita Loibok amesema agizo hilo litazingatiwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) ili mti huo uweze kuwa kivutio ndani na nje ya chini

ya nchi.

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles