» » Mwanamke ajaribu kugonga polisi akitumia gari Washington

Mwanamke ajaribu kugonga polisi akitumia gari Washington


Mwanamke ajaribu kugonga polisi akitumia gari WashingtonHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamke ajaribu kugonga polisi akitumia gari Washington
Polisi mjini Washington nchini Marekani, wamemfyatulia risasi mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari, baada ya yeye kugonga gari la polisi karibu na bunge la Marekani na baadaye kujaribu kuwagonga maafisa kadha wa polisi.
Mwanamke huyo hakupigwa risasi, kwa mujihu wa msemaji wa polisi mjini Washington.
Alikamatwa na kisa hicho kikasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya bunge.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya kugonga kwa magari miji ya London na Brussels,
Msemaji wa polisi Eva Malecki, amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na kisa hicho ni cha uhalifu.
Polisi wakiweka ulinzi katika bunge la MarekaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPolisi wakiweka ulinzi katika bunge la Marekani
Kisa hicho kilitokea wakati maafisa waligundua dereva ambaye alikuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida na kutaka kumsimamisha.
Dereva huyo kisha akageuza gari kwa haraka na nusura awagonge polisi.
Sababaua ya kisa hicho haijulikani na mwanamke huyo hajatambuliwa.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa kurudi eneo hilo.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440


BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en


tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles