» » Mwanamitindo agongwa na treni akipigwa picha Marekani

Mwanamitindo agongwa na treni akipigwa picha Marekani

Haki miliki ya pichaPRESS / PSALMS FUNERAL HOME

Mwanamke wa umri wa miaka 19, ambaye alikuwa anaanza kujikuza kama mwanamitindo, aligongwa na treni na kufariki alipokuwa anapigwa picha.

Fredzania Thompson alikuwa anapigwa picha hizo zake za mitindo, ambazo zilikuwa za kwanza, kwenye reli alipogongwa na gari moshi.

Picha za Thompson, alizopigwa muda mfupi kabla ya mkasa huo kutokea Navasota, Texas, zimesambazwa na familia yake.

Polisi wanasema alikuwa mjamzito wakati huo na kwamba alikuwa anaondokea treni moja kwenye njia moja ya reli alipojipata ameingia kwenye njia ya reli ambapo kulikuwa na treni nyingine iliyokuwa inapita ambayo ilimgonga.

Wafariki kwa kupiga 'Selfie'Agonga gari la polisi akijipiga selfieMtalii afa akijipiga 'selfie' Taj Mahal

Gazeti la The Eagle limesema ilikuwa mara yake ya kwanza kwenda kupigwa picha za uanamitindo.

"Bila shaka, hilo jambo alililotaka kulifanya maishani," Hakamie Stevenson alisema kumhusu bintiye.

"Ndiyo shughuli aliyoanza kuifanya siku aliyokumbana na mauti yake."

Polisi wanasema bado wanafanya uchunguzi kuhusu kisa hicho.

Afisa wa polisi wa Navasota ameambia BBC kwamba hata hivyo bado hawajagundua hila yoyote.

Haki miliki ya pichaPRESS/PSALMS FUNERAL HOMEImage captionFamilia ya Fredzania imetoa picha alizopigwa kabla ya kifo chake

Ukurasa umefunguliwa katika mtandao wa GoFundMe kujaribu kuchangisha $10,000 (£8,150) za kugharimia mazishi ya Fredzania.

Ajipiga risasi akitafuta 'Selfie ya mwaka'

Kwa mujibu wa shirika la reli la Marekani (FRA), watu 813 waliuawa kwenye reli Marekani mwaka 2016.

Hilo ni ongezeko la 8.45% ukilinganisha na mwaka 2015.

Mada zinazohusiana

MarekaniWanawake

Mshirikishe mwenzako 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles