» » Miili ya wataalamu wawili wa UN waliotoweka yapatikana DRC

Miili ya wataalamu wawili wa UN waliotoweka yapatikana DRC


Miili ya wataalamu wa UN yapatikana DRCHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMiili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC
Maafisa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanaamini kuwa wamepata miili ya wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa ambao walitoweka nchi humo.
Miili hiyo ilipatikana eneo ambapo raia wa Marekani Michael Sharp na raia wa Sweden Zaida Catalan walitekwa nyara wiki mbili zilizopita.
Miili hiyo ni ya mwanamume na mwanamke ambao wote ni wazungu.
Kumekuwa na ghasia eneo la Kasai, ambapo pia polisi 40 walipatikana wamekatwa vichwa mwishoni mwa wiki.
Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa walikuwa nchini DRC kufuatilia vikwazo vilivyowekwa dhidi DRC, lakini wakati huo walikuwa wakichunguza ripoti za dhuluma eneo la Kasai.
Msemaji wa serikali ya Congo Lambert Mende, alithibitisha ripoti za kupatikana kwa miili hiyo kwa BBC.
Hata hivyo amesema kuwa uchunguzi wa DNA unahitaji kuondoa shaka yoyote kuhusu miili hiyo.
Miili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC
Image captionMiili ya wataalamu wa UN yapatikana DRC
Serikali ya Congo inapigana na kundi la waasi ambalo linahudumu eneo hilo na linaaminiwa kuwateka wataalamu hao.
Ghasia eneo la Kasai zimechochewa kufuatia kuuliwa kwa kiongozi wa kitamaduni Kamuina Nsapu, ambaye alikuwa akiongoza upinzani dhidi ya Rais Joseph Kabila

Mada zinazohusiana

Tuma picha/ habari what-sap 0769436440

BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en

tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles