» »Unlabelled » Marufuku ya Laptopu na tabiti kuelekea Marekani yatekelezwa

Marufuku ya Laptopu na tabiti kuelekea Marekani yatekelezwa

Haki miliki ya pichaAFP/GETTYImage captionMwanaharakati wa Kuwait Thamer Bourashed akiweka laptopu yake ndani ya mzigo kabla ya kuabiri ndege

Marufuku ya laptopu na tabiti katika eneo la kubeba mizigo ya ndege zinazotoka Uturuki na mataifa mengine ya mashariki ya kati na yale ya Afrika Kaskazini imeanza kutekelezwa.

Maafisa wanasema kuwa vifaa hivyo ambavyo ni vikubwa ikilinganishwa na simu aina ya Smartphone havitaruhusiwa katika ndege ya abiria kwa kuwa huenda vinaweza kubeba vilipuzi.

Ni kampuni moja ya ndege pekee inayoruhusu vifaa hivyo kutumika hadi mtu anapoabiri ndege.

Uingereza yapiga marufuku laptopu ndani ya ndege kutoka nchi 6Marekani yapiga marufuku laptopu na tabiti kutoka mataifa 8Marekani yazuia abiria kubeba laptopu kutoka Misri na Morocco

Marufuku hiyo inasimamia mataifa manane huku Uingereza ikitoa marufuku kama hiyo vifaa hivyo kutoka kwa mataifa sita.

Kampuni tisa kutoka mataifa manane -Uturuki, Morocco, Jordan, Misri, UAE, Qatar, Saudia na Kuwait zimeathiriwa na marufuku hiyo ya Marekani.

Mataifa hayo huendesha safari 50 za ndege kuelekea Marekani.

Ndege za miliki ya kiarabu UAE hutoa huduma ya kusafirisha mizigo kupitia ndege na meli katika milango ya viwanja vya ndege ili kuwawezesha abiria kutumia vifaa vyao vya kielektroniki baada ya kuiingia katika eneo la kusubiri ndege hadi wanapoingia ndege.

Hiyo inamaanisha kwamba abiria wanaosafiri mara mbili kutoka mataifa mengine kuelekea Marekani kupitia Dubai wanaweza kutumia vifaa hivyo vya kielektroniki katika safari ya kwanza.

Marufuku ya Uingereza inaathiri ndege zote kutoka Misri, Uturuki, Jordan, Saudia, Tunisia na Lebanon.

Mada zinazohusiana

Marekani

Mshirikishe mwenzako

0769436440

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...