» » Job Ndugai aionya Serikali uwasilishaji wa mpango wa maendeleo

Job Ndugai aionya Serikali uwasilishaji wa mpango wa maendeleo


Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai ameionya Serikali juu ya ucheleweshaji wa uwasilishaji wa mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo waTaifa, kiwango na ukomo wa bajeti.

Akizungumza bungeni jana muda mfupi kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kuwasilisha mpango huo, Ndugai alisema kuwa kikanuni mpango huo unatakiwa kuwasilishwa Machi 11 ya kila mwaka.

“Kama ikiwa siku hiyo imeangukia siku isiyo ya kazi basi uwasilishaji huu hufanyika siku inayofuata. Mkija mwakani namna hii haitawezekana, hatutakuwa na mjadala,” alisema Ndugai.

Amewataka mawaziri, makatibu wakuu, maofisa wa Serikali na wabunge

kuhakikisha wanakuwapo mjini hapa kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa mpango huo kisekta na kuhakikisha kuwa kazi hiyo inakamilika kabla

ya kuanza kwa mkutano wa Bunge Aprili 4 mwaka huu.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440



BONYEZA HAPA KUPATA APP YA 4SN NEWS
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.sn.news&hl=en



tupe maoni yako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles