» » Jaji Gorsuch asema Trump hayuko juu ya sheria Marekani

Jaji Gorsuch asema Trump hayuko juu ya sheria Marekani

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionNeil Gorsuch alisema hawezi kupima maamuzi aliyowahi kuyatoa kwa mujibu wa uzito

Jaji aliyependekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kujaza nafasi iliyo wazi katika Mahakama ya Juu nchini humo, amesema hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria, hata Rais Trump aliyependekeza uteuzi wake.

Neil Gorsuch ameambia kikao cha bunge la Seneti kwamba hakuna mtu yeyote aliyemtaka kutoa ahadi kuhusu jinsi atakavyofanya maamuzi yake pindi atakapoidhinishwa kuwa jaji katika mahakama hiyo.

Amesema angekataa uteuzi huo iwapo Bw Trump angemtaka kubatilisha uamuzi wa kihistoria wa mahakama katika kesi Roe v Wade ambao ulihalalisha utoaji wa mimba.

Bw Gorsuch pia alishutumu vikali hatua ya Trump kuwashambulia kwa maneno majaji wa mahakama mara kwa mara na kusema "inavunja moyo".

Februari, rais huyo alimweleza jaji aliyebatilisha marufuku yake ya usafiri dhidi ya raia wa nchi saba kama "mtu huyo anayeitwa jaji".

Trump kuteua jaji anayepinga uavyaji mimbaTrump ayabana mashirika ya utoaji mimbaWatakaoumia na watakaofaidi chini ya Trump Marekani

Bw Gorsuch faraghani aliwaambia maseneta kwamba hilo lilikuwa na maana kwamba iwapo kungetokea shambulio la kigaidi katika ardhi ya Marekani, basi jaji huyo ndiye angekuwa lawamani.

"Mtu yeyote anapokosoa uaminifu na maadili au nia ya jaji wa mahakama, hilo linavunja moyo. Nafikiri linatamausha - kwa sababu naujua ukweli," alisema.

Alipoulizwa iwapo hilo linamhusu pia rais, alijibu: "Mtu yeyote ni mtu yeyote."

Msemaji wa ikulu ya White House Sean Spicer baadaye aliandika kwenye Twitjer kwamba Bw Gorsuch alikuwa akizungumza "kwa mapana" na kwamba hakumtaja mtu kwa jina."

Haki miliki ya pichaAFPImage captionMaandamano dhidi ya Neil Gorsuch 15 Machi

Wakati wa kikao chake cha kwanza kuhojiwa na maseneta, Gorsuch, ambaye ni jaji wa Colorado aliulizwa maswali mengi kuhusu msimamo wake.

Maseneta wa Democrat walisisitiza kuhusu baadhi ya mambo yenye utata, lakini alisisitiza mara kwa mara kwamba ingekuwa makosa kwake kueleza angetoa uamuzi wa aina gani katika kesi yoyote hilo.

Wasifu wa Trump, rais wa Marekani

Alisema huo ungekuwa ndio "mwanzo wa mwisho" wa mahakama huru.

Bw Gorsuch, amependekezwa kujaza nafasi iliyoachwa wazi kutokana na kifo cha Jaji Antonin Scalia miezi 13 iliyopita.

Mada zinazohusiana

Donald TrumpMarekani

Mshirikishe mwenzako 

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles