» » CIA kuchunguza iwapo Urusi ilingilia uchaguzi wa Marekani

CIA kuchunguza iwapo Urusi ilingilia uchaguzi wa Marekani

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionPicha ya rais Vladmir Putin na Donald Trump .Wapinzani wa Trump wanamtuhumu kuhusu uhusiano wake na Putin

Mwenyekiti wa kamati ya ujasusi katika bunge la Congress ambaye ni mwanachama wa Republican, Devin Nunes amesema wanachunguza ikiwa kulikua na ushirikiano wa kina kati ya Urusi na baadhi ya raia wa Marekani.

Taarifa hii inamaanisha kwamba suala la mchango wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani linaendelea kutiliwa manaani.

Kamati ya ujasusi katika baraza la Congress imekua ikiichunguza Urusi kwa miaka mingi na wakati huu inalenga kubaini ikiwa kulikua na shughuli zozote za Urusi katika uchaguzi wa Marekani .

Tayari Idara ya FBI inachunguza muingilio wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani.

Shirika la Ujasusi CIA na imekiri kwamba utawala wa Vladimr Putin ulinuia kusaidia Donald Trump kumharibia sifa mpinzani wake Hillary Clinton.

Donald Trump na timu yake wamekanusha kuwa baadhi ya watu kwenye timu ya Trump waliwasiliana na maafisa wa Urusi kabla ya Uchaguzi Mkuu.

Mshirikishe mwenzako

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles