MHUBIRI: Mchungaji David Mbaga
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
MAHALI: Kanisa la Waadventista Wasabato Mabatini Mwanza
Mafungu:1 Samwel 27:1-7;Walawi 19:27,28;Rumi 6:3,4;Mathayo 3:16;Mark 16:16
Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu”. (Yohana 3:5)
Watu wamekuwa na hofu na wakaingia katika mambo ambayo mwenyezi (Biblia)Mungu amekataza wakidhani wanatafuta amani pasipo mafanikio.Je ukitumia madawa ya kulevya utaondoa hofu?ulevi,ukahaba,starehe,kunyoa viduku utapata amani?habari gani ukichora mwili wako kwa tattoo ni salama kwako? Maandiko matakatifu yanakataa (Biblia)yanakataa katika (Walawi 19:27,28)
UKIKOSA AMANI HOFU IMETANDA UNAKWENDA WAPI? UNAKIMBILIA KWA WAFILISTI KAMA DAUDI?(1 Samwel 27:1-7)
Yesu Mfalme wa Amani aliye kufa na kufufuka anaondoa hofu zote kwa kila aaminiye na kubatizwa. Kumekuwepo na aina nyingi za Ubatizo ambazo ni kinyume na maagizo ya Mungu kama kunyunyiziwa maji kichwani,kupakwa mafuta,kuruka moto na nyingine nyingi. Ubatizo wa KWELI unapaswa kutanguliwa na Kuamini, Kutubu na kuungama.(Marko 16:16);Mathayo 3:6 inasema “naye AKAWABATIZA katika Mto yordani, huku WAKIZIUNGAMA DHAMBI zao” Matendo.2:38, “TUBUNI MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo”
Ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani kimsingi haufundishwi katika Biblia bali ni utaratibu ambao umewekwa na wanadamu tu. Kihistoria ulianza mwaka 1311 baada ya mkutano Wa RAVENA,kabla ya hapo wakristo walibatiza ubatizo Wa Biblia Wa watu wazima,na wakuzamisha katika maji mengi..
Katika lugha ya Kiyunani, ambayo ilitumika kuandikia Agano Jipya, kulikuwa na maneno yaliyotumika kwa kunyunyiza na kumwagia. Neno la kunyunyiza ni rhaino, kwa mfano neno hili lilitumika kwa ajili ya kunyunyiza damu. Neno kwa ajili kumwagia ni cheo. Ingawa maneno yote haya yalikuwepo wakati wa kuandikwa kwa Agano Jipya, hayakutumiwa kwa kuhusishwa na ubatizo. Badala yake neno lililotumika katika kwa kuhusishwa na ubatizo ni “baptisma”, ambalo lina mzizi wenye maana zamisha, tumbukiza au tosa.
Biblia inathibitisha kwamba mtu anamwamini kwanza YESU ndio anabatizwa.Kumbe kuwabatiza watoto ni matokeo ya kushindwa kuijua na kuielewa Biblia inavyotaka yenyewe na kufuata mapenzi ya wanadamu. Yohana hakumbatiza mtu ambaye hajatubu, ndio maana aliwahubiria kwanza wakatubu ndipo akawabatiza. Usikimbiekimbie kwa Wafilisti ifuate Biblia,Mungu wa kweli,Mfalme wa amani atakuondolea hofu na utakuwa mtu wa milki yake.
Tuma picha/ habari what-sap 0769436440
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment