Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imewazidi mahasimu wao, Simba na Azam katika orodha ya vilabu bora Afrika na Tanzania kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na mtandao wa FootballDatabase.
Kwa mujibu wa orodha hiyo, Yanga inaoongoza ubora Tanzania baada ya kujikusanyia pointi 1252 ikipanda kwa nafasi 14 huku ikimata nafasi ya 332 barani Afrika.
Azam wakisherekea ubingwa wa Mapinduzi
Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati, Azam wanashika nafasi ya pili nchini Tanzania kwa pointi zao 1249 na kukamata nafasi ya 353 barani Afrika.
Simba wanafunga orodha ya Tanzania katika nafasi ya tatu kwa pointi zao 1247 katika nafasi ya 358 barani Afrika. Hata hivyo Simba ndio timu iliyoimarika zaidi kwa kupanda kwa nafasi 38 toka nafasi waliyokuwa mwaka jana.
Mabingwa wa kihistoria Al Ahly wanaendelea kuongoza barani Afrika wakifuatiwa na Esperance de Tunisia, TP Mazembe, AS Vita na Etoile du sahel wakikamilisha tano bora.
Yanga yazikimbiza Azam na Simba kwa ubora Afrika
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment