» » Yanga kumalizana na Mwadui



Yanga kumalizana na Mwadui

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga leo watakuwa wenyeji wa Mwadui katika mchezo wa ligi utakaochezwa uwanja Taifa, Dar es Salaam.
Mara ya mwisho timu hizo zilikutana Septemba mwaka jana mjini Shinyanga katika mchezo wa raundi ya kwanza ambapo Yanga ilishinda mabao 2-0 yakifungwa na Amis Tambwe na Donald Ngoma.
Mchezo wa leo una umuhimu kwa kila mmoja kushinda Yanga ikitaka kuwa karibu na Simba kwa ajili ya kutetea taji lake na Mwadui ambao bado hawako katika nafasi nzuri wakihitaji pointi kujiweka sehemu salama.
Lakini Yanga inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo ikijivunia kuwa na kikosi bora kinachonolewa na Kocha Mkuu George Lwandamina na msaidizi wake Juma Mwambusi. Aidha, Mwadui inayonolewa na Kocha Ally Bushir ‘Bush’ina kazi kubwa ya kuhakikisha inapata pointi tatu ili kujiweka sehemu salama zaidi.
Kwa sasa Mwadui inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 22 na Yanga ikiwa na pointi 45 katika nafasi ya pili nyuma ya vinara Simba.
Yanga itaendelea kumkosa mchezaji wake tegemeo Donald Ngoma ambaye yupo kwao kwa matatizo ya kifamilia.
Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi alisema wako tayari kwa mapambano kuhakikisha wanashinda mechi zote kwasababu wanataka kutetea taji.
“Tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri, wachezaji wote wako tayari kwa mchezo. Tunaifahamu Mwadui sio timu rahisi wana wachezaji wazuri na wengine baadhi waliwahi kucheza Yanga, kwa hiyo utakuwa ni mchezo mgumu,”alisema.
Mechi nyingine itakayochezwa leo ni Majimaji ya Songea dhidi ya Ndanda kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Timu zote mbili haziko vizuri huku Majimaji ikishika nafasi ya pili kutoka mwisho kwa pointi 17 na Ndanda FC ikishika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 19. Kila mmoja anahitaji ushindi kuondoka kwenye hatari ya kushuka daraja.
CHANZO HABARI LEO 
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa WHATSAP (+255) 0769436440 Karibu Sana Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...