Amesema moja ya kati ya mambo yanayothibitisha kuwa Serikali ya awamu ya tano haina nia njema na wananchi wake, ni msimamo ilionao kuwa Taifa halina njaa.
Ntagazwa ambaye aliwahi kutuhumiwa kuwa si raia wa Tanzania licha ya kuwahi kutumikia wadhifa wa uwaziri katika serikali ya awamu ya kwanza mpaka ya tatu kabla ya kushinda kesi, ametoa kauli hiyo leo alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu.
“Kitendo cha Rais Magufuli kuwauliza wananchi wenya njaa kama wanataka akawapikie, kinasikitisha sana.
“Rais hawapikii wananchi chakula jikoni, bali anaangalia utaratibu wa kuwatafutia chakula cha msaada katika wakati wa njaa, lakini yeye ameng’ang’ania na kila sehemu anasema hakuna njaa,” amesema Ntagazwa.
Mwanasiasa huyo mkongwe amesema kuwa ametembea katika mikoa ya Simiyu na Mwanza ambapo kuna ukame, hakuna mvua na mazao ya chakula yamekauka sana.
“Wananchi ndiyo ‘mabosi’ na ili uwe kiongozi bora ni lazima uwasikilize watu, lazima ufike sehemu yote ya nchi na uangalie watu wanavyoishi kuliko kuzungumza tu,” amesema.
Kuhusu utumbuaji wa majipu unaoendelea, Ntagazwa amesema mara nyingi Rais Magufuli amekuwa akifanya maamuzi ya kufukuza watu kazi bila kufuata utawala bora, utaratibu na sheria za nchi.
“Utumbuaji majipu si ajabu lakini lazima watumishi waongozwe kwa kufuata utaratibu na sheria za nchi zilizopo, utumbuaji huu si mzuri kwani unasababisha watumishi wengi wa umma wafanye kazi kwa woga badala ya kufuata sheria na taratibu,” amesema Ntagazwa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment