» » Moto Wazuka Uwanja wa Ndege wa JNIA, Dar


 DAR ES SALAAM: Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno ameuambia mtandao huu kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

Aidha Meneja wa Uwanja huo ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za usafirishaji zimeamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika.

“Kwanza naomba niwatoe hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja wetu, ni kweli moto umezuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

“Lakini madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule terminal one (Uwanja wa zamani) zinaendelea kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.

“Baada ya kuudhibiti moto huo tumerudi kuangalia chanzo tukakuta, mfumo wa umeme uko sawa, hivyo hatujajua chanzo hasa cha moto huo ila tunajitahidi kufanya utafiti ili tujue.” Aliongeza Meneja na kusema taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.





Source: Global Publisher

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...