» »Unlabelled » KUCHEZA Dansi ndani ya KANISA kwenye Biblia!

Dansi ndani ya Biblia!


Uimbaji ni ibada ya kumsifu Mungu. Ni ibada kama zilivyo ibada nyingine kama kusoma/kujifunza Biblia, kuomba/kusali  nk. Kwa maneno mafupi, ni uijilisti unaoshughulika na nafsi ya mwimbaji/waimbaji wenyewe na wasikilizaji. Kwa sababu ni ibada nyeti sana, uimbaji unapaswa kufanywa kwa KICHO CHA UCHAJI MUNGU.
Dansi ndani ya Biblia.
Je, ndani ya Biblia kuna michezo au dansi? Kama ni ndiyo ni michezo au dansi gani na ilichezwa wapi? Chanzo chake kilikuwa ni nini?? Je, Biblia inaturuhusu kucheza?
Ndani ya Biblia kwa mara ya kwanza, wanawake wanaonekana wakicheza (Kutoka 15:20,21) Miriamu akiwa na tari mkononi mwake…(Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza, Miriamu akawaitikia…) Tunaambiwa kuwa Miriamu na wanawake wengine walicheza. Neno la kiebrania lililotumika hapa ni ‘ Mihola’ ambalo humaanisha kutembea katika duara. Pia chunguzza tafsiri ya Biblia ya King James Version imetumia maneno ya matari na machezo timbrels and dances/chuwls (vyombo vya kutoa sauti kwa kupuliza kama vile filimbi, vinubi nk). Mihola humaanisha kutembea(matching) kwenye  mistari miwili katika mduara.
Hivyo wanawake waliomfuata Miriamu nyuma walikuwa wakienda kwa matching na siyo kwa kurukaruka na kunengua viuno. Aidha, ikummbukwe kuwa, wanawake hawa hawakua kwenye ibada kanisani bali walikuwa safarini tu kutoka Misri utumwani kuelekea Kanaani. Maana iyohiyo ya neno hili ‘ Mihola’ limetumika pia katika 1 samweli 18:6 na Waamuzi 11:34.
Mbona kuna ibada za kucheza ndani ya Biblia?
Ni kweli. Katika Kutoka 32:6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze. Tukio hili lilifanyika baada ya uasi dhidi ya Amri za Mungu. Ndama alitengenezwa kinyume cha maagizo ya YEHOVA (Usijifanyie sanamu ya kuchonga…kutoka 20:4-6). Neno kucheza lilivyotumika hapa siyo sahihi. Neno la Kiebrania lililotumiwa hapa ni ‘ Sahak’  lenye maana ya kumcheka mtu fulani, kumdhihaki au kumtukana.
Hapa dhihaka ilikuwa ni kwa Mungu kwa sababu ilionekana kuwa Mungu ameshindwa kuwapeleka Waisraeli Kanaani na hivyo sasa waliamua kurudi Misri na mungu wao wa kuwarudisha huko alikuwa ni ndama wa dhahabu.  Wapendwa, kucheza dansi la Yesu ndani ya kanisa au ibada ni UASI.
Mbona Daudi alicheza mbele za Bwana??
Ni kweli. Katika 2 Samweli 6:14 tunasoma (Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani). Neno la Kiebrania lililotumika hapa ni ‘ karar’ lenye maana ya kurukaruka na kuzungukazunguka (leaping and whirling) na siyo sarakasi, minenguo ya viuno nk. Zingatia mambo yafuatayo kwa Daudi:
a.     Daudi hakuwa na maandalizi yoyote ya namna ya kucheza kama ilivyo leo kwa baadhi ya kwaya za injili kwenye makanisa yetu. Alirukaruka na kuzuzngukazunguka kama mtu anayepata furaha baada ya kufaulu mtihani, kupata mtoto, kupanda cheo nk. Ni furaha ya papo hapo tu. Daudi alipata furaha ya papo hapo tu na ambayo haikuwa endelevu kwa baadaye.
b.    Hakuwa na timu ya watu ambao walifanya maandalizi pamoja naye ya namna ya kurukaruka na kuzungukazunguka.
c.     Hakuwa hekaluni au kwenye mkutano wa ibada au mafundisho yoyote ya neno la Mungu. Daudi alijua fika kuwa ndani ya nyumba ya Bwana hakuna kurukaruka na kuzungukazunguka maana imeandikwa, Habakuki 2: 20 Lakini Bwana yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake
d.    Daudi hakucheza kama sehemu ya ibada mbele za Mungu
Na katika kitabu cha Zaburi 149:3 na 150:4 dhana  ya ‘maholi imejirudia tena hapa.’. Angali Zaburi
150: 3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa  kinanda na kinubi;
        4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
          (Mstari wa 4- kwa matari na machezo ambacho ni chombo                        
           cha muziki) 
NB:
Ikumbukwe kuwa neno kucheza kwa Kiswahili na dance kwa kiingereza hayana maaana sawa na ile iliyotumika kwenye lugha ya Kiebrania, lugha ambayo Biblia iliandikwa kwayo. Kwa mujibu wa zaburi na baadhi ya vitabu vingine ndani ya Biblia, neno kucheza lina maana ya “ maholi – matching katika mduara huku mkipuliza vyombo vya muziki vinvyotumika katika kumsifu Mungu.
Ieleweke kwamba, wahubiri na wanakwaya wanaosisitiza watu kucheza ndani ya hekalu au ibada, wako kwa ajili ya kutimiza kiu yao ya kucheza dansi ya dunia huku wakiivika dansi yao vazi la Kikristo. Kwa maneno mengine, kile kinachofanywa na watu hawa siku hizi ni “Upagani Mambo Kikristo”. Dhana ya uimbaji kama ibada ya kumtukuza Mungu haipo tena. Ibada ya uimbaji halisi alioneshwa nabii Isaya
Isaya 6: 2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
 3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
 4 Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi. 
Angali ndugu yangu mkristo, Malaika wamnamsifu Mungu kwa kufunika nyuso zao na miguu yao….  Ibada ya heshima kiasi gani!!!! Linganisha na leo watu wanavyovaa vimini, vitight nk halafu na kudansi madhabahuni eti wanamwimbia/kumchezea Mungu!!! Mimi nesema kuwa ni kweli wanamchezea (kwa maana ya kudhihaki na kumbeza) Mungu. Lakini wakumbuke kuwa Mungu hadhihakiwi…
Kama unamchezea Bwana, acha. Fuata taratibu nzuri za kibiblia za kumsifu Mungu kwa njia ya nyimbo na si vinginevyo.
Mwisho Shetani amefanikiwa hata kuichakachua Biblia. Biblia hiyohiyo uliyo nayo, HAIKO SALAMA NDG YANGU. Nakuchokoza kidogo tu. Hebu jaribu kulinganisa mafungu haya;
KJV-King James Version           NIV-New International Version    RSV-Revised Standard Version
Mathayo 24:36                                          Mathayo 24:36              Mathayo 24:36
Warumi 8:1                                              Warumi 8:1                    Warumi 8:1
1 Yoh 5:8                                                 1 Yoh 5:8                       1 Yoh 5:8
Je, mafungu yote haya, yanafanana???  Kama sivyo ni kwa nini?? Je, unafikiri Biblia ya Kiswahili ilitafsiriwa kwa kutumia Biblia gani kati ya hizo hapo juu??? Usiwe KINDA, chunguza na wewe!!
Naomba kuwasilisha!!
Michael Nzala
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...