» » Godbless Lema Arudishwa Tena Gerezani

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, leo imeshindwa kusikiliza rufani ya Jamhuri dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupinga dhamana yake, baada ya mawakili wa Serikali kuwasilisha notisi ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa wakipinga kusikilizwa kwa rufani hiyo .

Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Salma Maghimbi   alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa ya Jamhuri iliyopinga  Lema kupatiwa dhamana Novemba 11 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Desderi Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ambapo siku hiyo Jamhuri iliwasilisha notisi ya mdomo.

Baada ya Lema kufikishwa mahakamani saa 3.25 asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali, huku pia polisi wakiwa wametanda viwanja vya Mahakama Kuu ndani na nje sanjari na gari moja la maji ya kuwasha, baada ya  mawakili wa pande zote kujitambulisha Jaji Maghimbi alisoma notisi ya Jamhuri kupeleka shauri hilo Mahakama ya Rufaa na kueleza kufungwa kisheria kutoa uamuzi wa rufani hiyo.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...