Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk Ali Mohammed Shein na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad jana walihitimisha kampeni za vyama vyao za ubunge wa Dimani ambao uchaguzi wake unafanyika leo kila mmoja akitamba kushinda.
Dk Shein ambaye ni Rais wa Zanzibar, akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Fuoni alirejea kauli yake kwamba hakuna umoja wa mataifa au nchi yoyote inayoweza kumuondosha madarakani.
Dk Shein alisema hayo akiendelea kujibu kauli ya Maalim Seif kwamba siku si nyingi kutatokea mabadiliko makubwa na kwamba wanachama wake wasifadhaike.
Dk Shein alisema CUF walikataa wenyewe kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016, hivyo wanabaki wakitangatanga, “…Wasahau kabisa kuipata nafasi ya urais wa Zanzibar. Hawana uwezo hata wa kuongoza udiwani sembuse urais.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment