» » Bidhaa za Mexico kutozwa kodi Marekani, kufidia ukuta

Bidhaa za Mexico kutozwa kodi Marekani, kufidia ukuta




Rais wa Marekani na MexicoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais wa Marekani na Mexico

Ikulu ya Marekani imesema Rais wa nchi hiyo Donald Trump anaweza kutoza asilimia 20 ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Mexico kuweza kusaidia mpango wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili kuzuia kuingia kwa Wahamiaji haramu na madawa ya kulevya.
Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena Nieto kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini Washngton.
Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia mtangulizi wake Vicente Fox.
Bwana Fox amesema ana uhakika Mexico italipiza kisasi kwa kutoza kodi bidhaa zitokazo Marekani, iwapo mipango hiyo ya Rais Trump itatimizwa.
Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump. Katika ziara yake nchini Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.
Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia.

Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...