» »Unlabelled » Alama na Sanamu ya Mnyama


Alama na Sanamu ya Mnyama

Mnyama na Sanamu yake
Wengi wamekuwa na maswali yasiyo na majibu juu ya namba 666 kama ilivyoandikwa kwenye Biblia-Ufunuo 13 : Na wengine wamekuwa wakinyoshea kidole kuwa dhehebu fulani ni 666. Na wengine wakisema, kusali Jumapili ndiyo alama ya mnyama(666). Na wengine wameitafiri 666 kwa mitazamo yao wenyewe ili kulinda maslahi yao binafsi.
Niijuavyo mimi binafsi namba 666 kwa mujibu wa Biblia, nitaieleza ndani ya makala hii, na kama kutaonekana kuna upungufu wa njisi nitakavyoieleza, basi nitashukuru wadau mkitoa michango yenu ili kuongeza nyama kwenye mada hii. Na endapo kutaonekana makosa ya kitafsiri, nitafurahi kupokea miongozo ya wadau, lengo likiwa ni kuleta uelewa na ufahamu wa hoja hii tete miongoni mwa baadhi ya watu.
Wapendwa 666 ni mfumo/mamlaka inayoendeshwa na mkuu wa dunia hii yaani Lusifa. Mamlaka hii ina mtekelezaji wake wa majukumu hapa chini ya jua. Majukumu ya mamlaka hii ni kumpinga Mungu na sera zake zote. Kama tujuavyo wote, Mungu ni wa utaratibu, mamlaka hii inatangua taratibu zote za Mungu na kusimika zingine yaani bandia.
Kwa sababu hoja hii iko kwenye unabii sana, ndugu mkristo, nakupa mwongozo wa kuufahamu unabii ndani ya Biblia ili uijue zaidi 666 kuwa ni nini!
Ndani ya Biblia, ukikuta maneno haya yafuatayo(a-d) kiunabii, huwa yanabeba maana zilioneshwa mbele yake. Nimesema ni katika mazingira ya kiunabii tu, mahali pengine huendelea kuwa na maana zake za kawaida.
a. Bahari, humaanisha watu ufunuo 17:15
b. Upepo, humaanisha vita Yeremia 49:36-37
c. Wanyama, humaanisha falme/tawala Daniel 7:17
d. Pembe, humaniisha mtawala/watawala/mamlaka uf 17:16
Baada ya mwongozo huo, tuanze kuitafuta sasa 666 ndani ya Biblia kuwa ina maana gani.
Danieli 7:3-4 Ndipo wanyama wakubwa wanne wakatoka baharini, wote wa namna mbalimbali. Wa kwanza alikuwa kama simba, naye alikuwa na mabawa ya tai; nikatazama, hata mabawa yake yakafutuka manyoya, akainuliwa katika nchi, akasimamishwa juu kwa miguu miwili kama mwanadamu; naye akapewa moyo wa kibinadamu.
1. Simba anawakilisha utawala wa Babeli uliotawala miaka 605-539 KK
(KK= Kabla ya Kristo)
Danieli 7: 5 Na tazama, mnyama mwingine, wa pili, kama dubu, naye aliinuliwa upande mmoja, na mifupa mitatu ya mbavu ilikuwamo kinywani mwake katika meno yake; wakamwambia mnyama huyo hivi, Inuka, ule nyama tele.
2. Dubu anawakilisha Umedi na Uajemi uliotawala miaka ya 539-331KK
Daniel 7:6 6 Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.
3. Chui anawakilisha utawala wa Ugiriki/Uyunani uliotawala miaka ya 331-168 KK
Daniel 7:7 Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi. 8 Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
4. Mnyama wa kutisha anawakilisha utawala wa Rumi uliotawala miaka ya 168-436 BK
5. Pembe 10 huwakilisha falme 10 zilizoanza kutawala kuanzaia miaka ya 476 BK – hadi kurudi kwa Yesu mara ya pili.
Tawala hizo ni zipi ndani ya utawala wa mnyama wa nne??
1. Heruli
2. Vandals Hawa wote waling’olewa Dan. 7:8
3. Ostrogoths
4. Alamani – bado wapo, leo wanajulikana kama Wajerumani
5. Burgundians – “ “ “ Waswisi
6. Franks – “ “ “ Wafaransa
7. Lombatis – “ “ “ Wataliano
8. Saxons – “ “ “ Waingereza
9. Suevi – “ “ “ Wareno
10. Visigoths – “ “ “ Wahispania
Rejea tena : Daniel 7:8
Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang’olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.
Sifa za pembe ndogo (Rumi ya kisiasa na kidini)
1. Iliinukia kati ya pembe 10 (yaani Rumi)
2. Iliinuka baada ya pembe 10 (yaani utawala wa Rumi)
3. Ina nguvu za kisiasa na za kidini
4. Ina uwezo wa kivita –maana ilipindua pembe 3 za mwanzo
5. Ina mcho ya mwanadamu – ishara ya akili na hekima nyingi
6. Itanena MAKUFURU dhidi ya YEYE ALIYE JUU (YEHOVA)
666 ni mfumo uliotawala (mnyama namba 4 tajwa hapo juu)na utakaotawala dunia yote ambapo utekelezaji wa sheria zake utafanywa na mataifa makubwa. Mfumo huu ni Rumi iliyotawala enzi za mitume na kuwaua. Mamlaka hii itatawala tena muda si mrefu na kuwatesa hata kuwaua wale watakaong’ang’ana na kweli ya Biblia kama mitume wa Yesu. Biblia inasema jeraha lake likapona tena… Ufunuo wa Yohana 13:12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona. Underground societies zilizo chini ya mamlaka hii ni vyama 10 vya siri) ikiwemo freemason-wajenzi huru.
666 ni jina la mtawala wa mamlaka hii duniani, yaani anajulikana kwa jina la “Mwakilishi wa Mwana wa Mungu” duniani. Mwakilishi huyu, atakuwa na mamlaka tena ya kusamehe watu dhambi kama alivyofanya enzi za mitume. Angalia maana yake (mwakilishi wa Mwana wa Mungu).
VICARIUS FILII DEI
(Mwakilishi wa Mwana wa Mungu)
“hata ile sanamu ya mnyama inene Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake. Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.”Ufunuo 13 :15-18 Linganisha na Daniel 7.
Kwa mujibu wa ufun 13 fungu la 17, kuna sifa 3 muhimu za kumtabulisha
¨ Alama yake (Mamlaka yake)
¨ Jina lake
¨ Namba ya jina lake (666).
Alama ya Mamlaka ya Rumi- Jumapili
Angalia maana ya jina lake kwa Kigiriki = LATEINOS
¨ L = 30 lambda
¨ A = 1 alpha
¨ T = 300 tau
¨ E = 5 epsilon
¨ I = 10 iota
¨ N = 50 nu
¨ O = 70 omicron
¨ S = 200 sigma
————
666
Rejea hapa Encyclopedia Britannica under “Languages of the World”, Table 8.
Maana ya Kimaandishi:
VICARIUS – Asimamaye badala ya, au kwa
niaba ya.
FILII – Mwana/kijana wa kiume
DEI – Maana yake ni MUNGU
Ufafanuzi wa jina lenyewe
V = 5 F = no value D = 500
I = 1 I = 1 E = no value
C = 100 L = 50 I = 1
A = no value I = 1 501
R = no value I = 1
I = 1 53
U/V = 5
S = no value
112
Haya fanya mahesabu rahisi tu 112 + 53 + 501 = 666
Sasa, jiulize ni mfumo gani wa imani duniani ambao viongozi wake wana mamlaka ya kusamehe watu dhambi? Na ndiyo mfumo huuhuu unaozungumziwa ktk Daniel 7 :25 « …naye atabadili sheria na majira…). Angalia Rumi ilifanya nini kwenye sheria za Mungu na majira ?
Mf. > Sheria zote za maadili(yaani Amri 10 za Mungu) amerekebisha zote
na ya nne akaitoa kabisa.
Angalia mwanzo wa siku kibiblia na kisha ulinganishe na kidunia.
Angalia siku za mwezi ndani ya Biblia kisha linganisha na za dunia
Angalia tunavyoandika saa na mwonekano wake nk
Badala ya watu kumwabudu Mungu wa mbinguni (Yahwe), wamegeukia ibada za jua (sun + day = Sunday) makanisani, huku wakifundishwa kuwa wanamwabudu Mungu kumbe sivyo(Soma Ezekiel 8:13-18). Hapa kuna historia ndefu. Chimbua na wewe!
13 Akaniambia tena, Utaona tena machukizo makubwa mengine wanayoyatenda. 14 Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi. 15 Akaniambia, Mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo. 16 Akanileta mpaka ua wa ndani wa nyumba ya Bwana, na tazama, mlangoni pa hekalu la Bwana, kati ya ukumbi na madhabahu, walikuwako watu kama ishirini na watano, wamelipa kisogo hekalu la Bwana, na nyuso zao zimeelekea upande wa mashariki, nao wanaliabudu jua, kwa kuuelekea upande wa mashariki.17 Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa? Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha; na, tazama, wanaliweka tawi puani. 18 Kwa sababu hiyo mimi nami nitatenda kwa ghadhabu; jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma, na wajapolia masikioni mwangu kwa sauti kuu, sitawasikiliza.
Uthibitisho mwingine wa Daniel 7:25 ya kwamba ni Rumi
“Who Changed the Sabbath”
1. Sylvester the pope first among the Romans . . . ordered that the rest (otium) of the Sabbath would better be transferred to the Lord’s day, so that we should leave that day free of worldly works in order to praise God.—Rabanus Maurus, De Clericorum Institutione, bk. 2, ch. 46; found in Bible Student’s Source Book, entry 1765.
2. Ushahi mwingine; In the early part of the fourth century the emperor Constantine issued a decree making Sunday a public festival throughout the Roman Empire. . . . He was urged to do this by the bishops of the church, who, inspired by ambition and thirst for power, perceived that if the same day was observed by both Christians and heathen, it would promote the nominal acceptance of Christianity by pagans and thus advance the power and glory of the church.—Great Controversy, p. 53.
3. She thus agrees with what Catholic writers have said on the matter. They attribute the change of the Sabbath to Sylvester I, bishop of Rome in the time of Constantine, and she connects bishops of that time period with the very first Sunday law, the one passed by Constantine. This harmonizes with Bacchiocchi’s own research:
Mosna finds a “fundamental reason” in the fact that the Church “influenced Constantine’s decision to make Sunday a day of rest for the whole empire, and this undoubtedly in order to give to the Lord’s day a preeminent place above the other days.“From Sabbath to Sunday, p. 315.
4. Swali: Siku ya Sabato ni ipi?
Jibu : Jumamosi ndiyo siku ya Sabato.
Swali : Kwa nini tunaabudu jumapili badala ya jumamosi ?
Jibu : Kwa sababu kanisa la katholiki lilihamisha utukufu kutoka
jumamosi kwenda jumapili.
The Convert’s Catechism of Catholic Doctrine by P. Gieremean 1977 pg 50
Hivyo basi, mfumo wa katholiki ndiye mpinga Kristo na jina lake ndilo 666. Chapa ya mnyama ni mafundisho yaliyo kinyume na yale ya Biblia, yaani Babeli(machafuko). Hakuna 666 atakayowekewa mtu usoni au kwenye mkono wake wa kuume. Hii ni lugha ya kinabii tu yenye maana kwamba, Kupokea 666 usoni ni kuitambua mamlaka hiyo akilini au mawazoni mwa watu kuwa ndiyo mamlaka pekee ya Mungu kinyume na Biblia inavyosema. Kuipokea 666 kwenye mkono ni kunyosha mkono yaani kutoa ukubali wa kufuata mafundisho ya Babeli. Kusali J2, siyo alama ya mnyama kwa sasa maana mlango wa rehema haujafungwa. Bado sauti ya tokeni kwake enyi watu wangu inaendelea kusikika….Ufunuo 18 :4. Mlango wa rehema ukifungwa, wanaosali j2 watakuwa wameshapokea alama ya mnyama tayari.
Kusema kweli kwa sasa, bado kabisa hatujapigwa ile chapa ! Nasema maana mlango wa rehema haujafungwa. Siku serikali ya dunia (Marekani) ikitangaza kuwa watu wote kwa dini zao wasali j2(wapumzike j2 peke yake), hapo ndipo alama ya mnyama(kupigwa chapa) itakapoanza kufanya kazi. Hatari ni kwamba, tangazo hilo likitokea unaweza kukutwa bado uko kule, au ulishakufa ukiwa huko uliko. Hii ni hatari kubwa sana. Madhehebu yote duniani yameshaungana (kasoro wasabato) na bado kidogo tu moto uwake. Kwa maelezo zaidi bofya hapa : http://www.oikoumene.org/en/member-churches.html
Ubarikiwe unapotafakari na kuchimba zaidi ili ufahamu then, ufanye uamuzi
Barikiwa
” 6 Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye Injili ya milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
7 akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
8 Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake.
9 Na mwingine, malaika wa tatu, akawafuata, akisema kwa sauti kuu, Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake,
10 yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake; naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika watakatifu, na mbele za Mwana-Kondoo.
11 Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na kila aipokeaye chapa ya jina lake”. Ufun. 14:6-11
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...