» » Afande Sele Awaomba Msamaha Mashabiki zake

BAADA ya kutangaza kuachana na siasa, mwanamuziki wa Hip Hop, Selemani Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na kuwaomba msamaha mashabiki zake aliowakwaza kipindi yuko kwenye siasa na sasa alivyojiondoa.
Akizungumza na Gazeti la Risasi Jumamosi, Afande Sele alisema anawaomba msamaha wote kutokana na kuingia na kutoka kwenye siasa hivyo wamuunge mkono kwenye muziki kwani amerudi rasmi.
“Nawaomba mashabiki zangu wanisamehe, wanipokee kwa mara nyingine kwenye muziki kwani nakuja na kazi mpya nzuri, nguvu zote nimezielekeza kwenye muziki sasa,” alisema Afande Sele.
Hivi karibuni Afande Sele ambaye alikuwa ni mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo pia aligombea ubunge kwenye uchaguzi uliopita, alitangaza kuachana na siasa na kurudi rasmi kwenye muziki

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...