» »Unlabelled » Wabunge wapigana tena nchini Kenya

Wabunge wapigana tena nchini Kenya


Wabunge wa upinzania nchini Kenya CORD muda mfupi baada ya kutoka ndani ya bunge kwa hasira
Image captionWabunge wa upinzania nchini Kenya CORD muda mfupi baada ya kutoka ndani ya bunge kwa hasira
Wabunge wa upinzani nchini Kenya wametoka bungeni kwa hasira katika mji mkuu wa Nairobi, wakisema kuwa baadhi yao walinyanyaswa bungeni mapema asubuhi.
Kikao hicho maalum ambacho vyombo vya habari havikuruhusiwa kuingia kilitarajiwa kupigia kura marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambayo inaruhusu kuhesabiwa kwa kura moja baada ya nyengine katika uchaguzi wa urais mwaka ujao.
Serikali inataka mfumo ambao utasaidia shughuli ya kuhesabu kura iwapo mfumo wa kielektroniki utafeli lakini upinzani unasema kuwa ni njia moja ya kuiba kura.
Awali hatua ya kuupigia kura mswada huo ili ufanyiwe marekebisho ilisababisha kuzuka kwa ghasia siku ya Jumanne.
Upinzani wa CORD umesema kuwa mmoja ya wabunge wake alivuja damu usoni kufuatia mgogoro na wabunge wa chama tawala mapema siku ya Jumatano.
Cord imeenda mahakamani ikitaka marekabisho hayo kutopitishwa bungeni lakini chama tawala kimepitisha marekebisho hayo.
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena Read More

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...