» »Unlabelled » Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini Park Geun-hye

Wabunge wapiga kura kumfuta rais wa Korea Kusini Park Geun-hye



Waandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakutaka Bi Park aondolewe madarakaniImage copyrightAFP/GETTY IMAGES
Image captionWaandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani

Wabunge nchini Korea Kusini wamepiga kura kumuondoa madarakani Rais wa Park Geun-hye.
Hoja hiyo imepitishwa na wabunge 234 dhidi ya 56.
Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.
Hatua hiyo itamlazimisha Bi Park kung'atuka kwa muda huku Mahakama ya Kikatiba ikiamua iwapo ataondolewa kabisa kutoka wadhifa huo wa urais.
Suala kuu limekuwa ni uhusiano kati ya Bi Park na msiri wake mkuu Choi Soon-sil, ambaye anadaiwa kutumia uhusiano huo kujizolea ushawishi nchini humo.
Viongozi wa mashtaka wanasema Bi Park alikuwa na "mchango mkubwa" katika visa kadha vya ufisadi, tuhuma ambazo amezikanusha.
Aidha, alikataa wito wa kumtaka ajiuzulu akisema uamuzi huo aliuachia bunge.

Bi Park amekataa wito wa kumtaka ajiuzuluImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionBi Park amekataa wito wa kumtaka ajiuzulu

Bunge la Korea Kusini lilianzisha hoja hiyo Alhamisi, ambapo iilihitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya wabunge ndipo kupitishwa.
Wachanganuzi walikuwa wanasema hilo lingekuwa jambo ngumu.
Bunge linatawaliwa na vyama vya upinzani na wabunge huru ambao wanataka aondolewe madarakani, lakini walihitaji wabunge 28 zaidi kutoka kwa chama cha Saenuri, chake Bi Park, ndipo wafikishe idadi ya kura inayohitajika.
Lakini matokeo yanaonesha wapo wabunge wa chama chake waliompinga.

Choi Soon-silImage copyrightAFP/GETTY IMAGES
Image captionBi Choi ni rafiki wa karibu wa Bi Park

Mada zinazohusiana

Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...