Kesi iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya Godbless Lema kuwa mbaya gerezani.
Taarifa za Godbless Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai kwa Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwezile ambapo alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza zikieleza kuwa mbunge huyo anaumwa na amepewa mapumziko hivyo asingeweza kufika mahakamani.
Aidha, taarifa kutoka kwa kiongozi huyo wa magereza hazikueleza wazi kuwa mbunge huyo anaugua ugonjwa gani.
Kuhusu kesi hiyo inayowakabili wanandoa hao wawili jana walikuwa wasomewe hoja za awali ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka upande wa Jamhuri, George Katabazi alikuwa atoe ushahidi.
Godbless Lema na Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha kitendo wananchodaiwa kuwa walikitenda kupitia ujumbe mfupi wa simu mara baada ya Rais Magufuli kumteua Mrisho Gambo kuuongoza mkoa huo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment