Arsenal wamaliza vinara kundi lao UEFA
Arsenal wamefanikiwa kuwaliza kileleni katika Kundi A Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kupata ushindi mkubwa dhidi ya FC Basel ya Uswizi.
Ufanisi huo ulitokana na mabao matatu aliyoyafunga kiungo Lucas Perez na kuwawezesha kushinda 4-1.
Wapinzani wao Paris St-Germain, ambao kabla ya mechi za Jumanne walikuwa wanaongoza kundi, walishuka na kumaliza nambari mbili baada ya kutoka sare na Ludogorets Razgrad wa Bulgaria mjini Paris.
PSG wangefanikiwa kumaliza vinara iwapo wangeshinda mechi hiyo, lakini hilo halikuwa.
Perez alifungua Arsenal mabao matatu nalo la nne likatoka kwa Alex Iwobi kabla ya Seydou Doumbia kufungia Basel bao la kufutia machozi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Arsenal kumaliza kileleni kundi lao tangu msimu wa 2011-12.
Hata hivyo, vijana hao wa Arsene Wenger hawakufanikiwa kusonga zaidi ya hatua ya 16 bora mwaka huo.
Wamekuwa wakiondolewa kwenye michuano hiyo hatua hiyo ya muondoano kila msimu kwa misimu sita iliyopita.
Kando na kufanikiwa kumaliza kileleni Gunners, pia wamefanikiwa kumaliza michuano ya hatua ya makundi bila kushindwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2005-06, msimu ambao walifika fainali.
Gunners' good fortune?
Drooo ya hatua ya makundi itafanyika Jumatatu na Arsenal wamefanikiwa kuwakwepa Barcelona na Monaco, waliowaondoa kwenye michuano misimu miwili iliyopita. Aidha, wamewahepa pia Atletico Madrid na Napoli.
Hata hivyo, wanaweza kukutana na mmoja wa hawa:
- Bayern Munich, waliowachapa 2013 na 2014
- Borussia Dortmund au Real Madrid
- Benfica
- Bayer Leverkusen
- Porto au FC Copenhagen
- OJuventus, Seville au Lyon
Watakaofuzu hatua ya Muondoano |
---|
Kundi A: PSG na Arsenal, Europa League (EL) - Ludogorets |
Kundi B: Benfica na Napoli, EL - Besiktas |
Kundi C: Barcelona na Manchester City, EL - Borussia Monchengladbach |
Kundi D: Atletico Madrid na Bayern Munich, EL - FC Rostov |
Kundi E: Monaco na Bayer Leverkusen |
Kundi F: Borussia Dortmund na Real Madrid |
Kundi G: Leicester na mmoja kati ya Porto na FC Copenhagen |
Kundi H: Juventus na mmoja kati ya Sevilla na Lyon |
Asante kwa kutembelea Blog yetu washirikishe na wenzako, Pia tunaomba maoni yako hapa au tupigie kwa (+255) 0769436440 Karibu Tena
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment