Samatta na Wanyama watemwa orodha ya CAF 2016
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya wachezaji watano watakaoshindania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2016, kwa wachezaji wa jumla na wachezaji wa ligi za barani Afrika.
Wanaoshindania tuzo ya jumla ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka ni:
- Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Borrusia Dortmund
- Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester
- Sadio Mane wa Senegal na Liverpool
- Mohamed Salah wa Egypt na Roma
- Islam Slimani wa Algeria na Leicester
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayechezea soka ya kulipwa Ubelgiji Mbwana Ally Samatta ni miongoni mwa wachezaji 30 waliokuwa wameteuliwa kushindania Tuzo ya shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ya Mchezaji Bora wa Afrika katika awamu ya kwanza kabla ya wachezaji hao kupunguzwa hadi watano.
Mkenya Victor Wanyama ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Tottenham alikuwa pia ameteuliwa, pamoja na Yannick Bolasie wa DR Congo anayechezea Everton.
Wachezaji watakaoshindania orodha ya Mchezaji Bora wa Afrika wa Mwaka anayecheza ligi za Afrika ni:
- Khama Billiat wa Mamelodi Sundowns na Zimbabwe
- Keegan Dolly wa Mamelodi Sundowns na South Africa
- Rainford Kalaba wa TP Mazembe na Zambia
- Hlompho Kekana wa Mamelodi Sundowns na South Africa
- Denis Onyango wa Mamelodi Sundowns na Uganda
Wachezaji hao waliamuliwa kwa kura zilizopigwa na Kamati ya Wanahabari ya CAF, Kamati ya Kiufundi na Ustawishaji ya CAF na nusu ya wanachama wa jopo la wataalamu 20.
Kwa awamu ya mwisho, kura za makocha wa timu za taifa/wakurugezi wa kiufundi wa mashirikisho 54 ya kitaifa yaliyo wanachama wa CAF pamoja na wanachama washirika - Visiwa vya Reunion na Zanzibar -, kwa pamoja na nsu hiyo nyngine ya wanachama wa jopo la wataalamu 20 zitahesabiwa kuamua washindi.
Mshindi atatangazwa Abuja, Nigeria Alhamisi, 5 Januari 2017
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment