*K E S H A LA A S U B U H I*
J'NNE OCT-11/2016
*NENO KUU 👇🏽*
*👉🏽TUNAKAA NDANI YA KRISTO👇🏽*
*_👉🏽Kunyauka kwa Tawi Kunamaanisha Kutengwa na Yesu_*
*Fungu la maandiko 👇🏽*
👉🏽 *_📝Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea._* *YOHANA - 15:6.*
🍂🍂🍂🍂🍂🍂🍂🍂
*_📕YEYE (Yuda)… HAKUBADILISHWA NA KUONGOKA na kuwa tawi lililo hai kwa njia ya muunganiko na Mzabibu wa Kweli. Mti huu mchanga haukushikilia Mzabibu hadi ulipokuwa tawi kubwa lenye kuzaa matunda. Alidhihirisha kwamba yeye alikuwa pandikizi ambalo lisingezaa tunda, -- pandikizi ambalo halikuungana na Mzabibu; nyuzi kwa nyuzi na vena kwa vena ili kuwa mshirika wa uzima wake._*
*_Mti mchanga ulio mkavu, usio na mwunganiko, unaweza kuwa na umoja pamoja na shina la mzabibu mkuu kwa kuwa tu mshirika wa uzima na lishe ya mzabibu ulio hai, kwa kupandikizwa kwenye mzabibu, kwa kuletwa kwenye uhusiano wa karibu inavyowezekana… Kitawi kinakuwa kikishikilia mzabibu unaotoa uzima, hadi uzima wa mzabibu unapokuwa uzima wa tawi na kuzaa tunda kama lile la mzabibu._*
*_📙Kristo alisema, “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi.” 🍒🍒 Mwunganiko wa karibu zaidi unaoneshwa kwa kielelezo hiki. Pandikiza kitawi kisicho na majani kwenye shina la mzabibu unaoshamiri nacho kitakuwa tawi lililo hai, kikichukua utomvu na lishe kutoka kwenye mzabibu. Uzi kwa uzi, vena kwa vena, ule mti mchanga unashikilia, hadi unapochipua na kuchanua na kuzaa matunda. Kitawi kikavu – kisicho na utomvu 🍂 kinawakilisha mwenye dhambi. Anapounganika na Kristo, nafsi inakuwa imeunganika na nafsi, aliye mnyonge na mwenye ukomo anaunganika naye aliye mtakatifu na asiye na ukomo na mtu anakuwa mmoja pamoja na Kristo._*
*_📕Tawi linaloonekana kuwa kavu, 🍂 linapounganika pamoja na mzabibu ulio hai, 🍒 linakuwa sehemu yake…. Nafsi, inapokufa katika uasi na dhambi, lazima ipitie uzoefu wa mchakato huo… Kama pandikizi linavyopokea uzima linapounganishwa na mzabibu, vivyo hivyo mwenye dhambi anashiriki tabia ya Mungu anapounganishwa na Kristo. Mwanadamu ambaye ana ukomo anaunganika na Mungu asiye na ukomo. Mwunganiko huo unapotokea, maneno ya Kristo yanakaa ndani yetu nasi hatusukumwi na hisia za kushtukiza, bali na kanuni iliyo hai inayodumu._*
*………………………🔚………………………*
*MUNGU AKUTIE NGUVU UWE IMARA*…… 🙏🏾
🍂
🍂

No comments:
Post a Comment