» »Unlabelled » Vikosi vya ulinzi na usalama vyaendesha mafunzo

Vikosi vya ulinzi na usalama vyaendesha mafunzo

FRIDAY , 23RD SEP , 2016

Vikosi vya ulinzi na usalama vimefungua mafunzo ya pamoja ya utendaji kivita kwenye maeneo ya fukwe na visiwa vilivyopo ndani ya bahari kwa lengo la kukabiliana na maovu yatendekayo ndani ya bahari na kuimarisha ulinzi.

Jenerali Davis Mwamunyange - Mkuu wa Majeshi (JWTZ)


Mafunzo hayo ya pamoja ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya JWTZ yameshirikisha vikosi vya Anga, Nchini Kavu na Baharini, JKT na Wanamgambo kwa lengo la kuwajengea uwezo kivita na huku ikielezwa kuwa Jeshi la Tanzania ni miongoni mwa majeshi bora dunia.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema jeshi limekuwa imara katika kuhakikisha linakabiliana na vitendo vya uharamia, ugaidi, uvuvi haramu na uingizwaji wa madawa ya kulevya na uhalifu wowote unaoweza kutokana na fukwe zetu.

Mafunzo hayo yatahitimishwa Wilayani Bagamoyo Septemba 30 na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku Kaimu Mkuu wa Kamandi ya Wanamaji akiwataka watanzania kutambua kuwa Jeshi lao lipo imara katika kulinda mipaka

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles