» »Unlabelled » Jeshi la Syria limetangaza kuanza tena mapigano makali

Jeshi la Syria limetangaza kuanza tena mapigano makali


Mapigano mapya SyriaImage copyrightAFP
Image captionMapigano mapya Syria
Jeshi la Syria limetangaza kuwepo kwa mapigano mapya makali, kutaka kurudisha eneo linalodhibitiwa na waasi huko Aleppo, ambako takriban watu laki mbili na nusu wamezingirwa.
Jeshi hilo limewataka pia raia kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Limesema njia za kutoka katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi zimewekwa wazi kuruhusu watu kutoka.
Tangazo hilo limekuja siku chache baada ya kushambuliwa kwa eneo hilo linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa Allepo.
Katika hatua nyingine Marekani na Urusi zimeshindwa kukubaliana jinsi ya kuufufua upya mkataba wa kusitisha mapigano, nchini Syria.
Akizungumza baada ya mkutano wao mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry amesema Urusi inatakiwa kuonesha umakini wake katika kumaliza ghasia nchini Syria.
''.. Iwapo Urusi itatujia na mapendekezo yenye kujenga tutawasikiliza. Watu wanahitaji kuamini kwa vyovyote vile inastahili kubadilisha mbinu za upigaji mabomu uliopo sasa ambazo zinaleta maafa na zenye kutatiza, kwa kubadili mbinu hizo tunaweza kupata ufumbuzi...''
Amesisitiza kuwa njia pekee ya kuonesha uaminifu ni kuacha mashambulizi ya nga, vinginevyo amesema mazungumzo mengine yatakuwa hayana msingi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU WATARIFU NA WENZAKO PIA TUPIA MAONI YAKO

Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About IVST TANZANIA

Hi my name is Gasto Alex Didas
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...

Popular Articles