Makamu wa Rais kufunga Nanenane
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga Maonesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane), yanayofanyika kitaifa kwenye Viwanja vya Ngongo katika Manispaa ya Lindi.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Makamu wa Rais, aliwasili Lindi mchana jana akitokea Dar es Salaam kwa njia ya barabara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Samia anatarajiwa kufunga maonesho hayo ya Nanenane kwa niaba ya Rais John Magufuli.
Alipowasili Ikulu ndogo mjini Lindi, Makamu wa Rais alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa.
Katika msafara wake, Makamu wa Rais amefuatana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment