» »Unlabelled » Maafisa 150 serikalini wahusishwa na mihadarati

Maafisa 150 serikalini wahusishwa na mihadarati



Rodrigo Duterte akitaja majina ya maafisa wakuu wanaohusika na mihadaratiImage copyrightEPA
Image captionRais Duterte amesema kuwa atachukuwa lawama zote endapo yeyote aliyetajwa atapatikana bila makosa

Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, amewataja hadharani na kuwahusisha maafisa wakuu wa serikali yake na ile ya awali na mtandao mpana wa ulanguzi wa dawa za kulevya nchini humo.
Rais Rodrigo Duterte, amewataka wajisalimishe kwa idara ya usalama inayopamban na ulanguzi wa mihadarati la sivyo watachunguzwa.
Wakuu hao ni pamoja na mameya, wabunge na majaji wa taifa hilo.
Anasema wote hao wanahusika na biashara hiyo haramu.
Katika hotuba kwa taifa iliyopeperushwa moja kwa moja kwa runinga, Rais Duterte amewaomba wenyewe wajitokeze na kuingia korokoroni kabla hajawakamata.
Rais huyo alisoma majina yao moja baada ya mwengine na mara moja akaamrisha maafisa wanaowapa usalama wajiondoe mara moja.
''Wale watakaoonesha japo dalili ya kupinga kukamatwa ninawaamrisha polisi kuwafyatulia risasi papo kwa hapo'' aliongezea kiongozi huyo.
Rais huyo alitwaa mamlaka mwezi Juni mwaka huu huku akiapa kukabiliana vilivyo na tatizo la ulanguzi wa mihadarati.
Inaaminika kuwa mamia ya watu wanaoshukiwa kuhusika na biashara hiyo haramu wameuwawa na maafisa wa polisi katika siku za hivi karibuni.

Pakua App Yetu-Bofya Hapa Flower
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

About 4sn News

Hi my name is Gasto Alex Didas from Mwanza Tanzania I'm blog manager and I have an App which is called 4sn News, my office is located in Rock City Mwanza-Tanzania at Miembeni "B" Street. My contacts +255769436440/ +255659750504 Welcome.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Popular Articles

MBUNGE MABULA AKAGUA SHULE NNE MPYA ZA MSINGI, ZENYE THAMANI YA TSH 1.174 BIL, ASHAURI HALMASHARI KUTUMIA MCHORO MPYA WA TAMISEMI KUOKOA MADARASA 3 KILA SHULE

Mhe. Stanslaus Mabula Mbunge Jimbo La Nyamagana amefanya ziara ya kikazi katika Kata nne za halmashauri ...